text string |
|---|
Kwa hiyo tumpongeze sana Mheshimiwa Rais na kwa kweli tuna imani kwamba baada ya muda mfupi maendeleo yatakayokuwepo katika nchi yetu, yatakuwa ni ya kuigwa kwa Nchi za Afrika, lakini hata katika dunia yetu hii. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nijielekeze katika eneo la barabara. Sote tunatambua kuna mvua kubwa... |
Hii imepelekea kuandika ombi maalum kwa watu wa TARURA watusaidie walau hata bilioni 2.5 kwa ajili ya kuhakikisha tunarudishia miundombinu, kwa sababu zaidi ya kata sita sasa hazina mawasiliano kabisa. Tunaishauri Serikali ifanye jitihada kubwa za kuhakikisha kwamba inarudishia miundombinu hii ili jitihada za kimaendel... |
Sasa tunayo Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 – 2020, hii Barabara ilikuwemo, ni moja kati ya barabara ambayo haikutekelezwa katika miaka mitano ile. Tumekuja 2020 – 2025, leo tunakwenda mwaka wa nne barabara hii haijatekelezwa japokuwa imo katika mpango wa bajeti mpaka hivi tunavyozungumza. Hili halileti... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, katika ilani tumebainisha kwamba kuna haja ya kuunganisha wilaya na Makao Makuu ya Wilaya na Mawa. Nataka nitoe taarifa, kwa kweli sitasita kushika shilingi katika bajeti ya Wizara hii ambayo inahusiana na ujenzi kuhusiana hili la kutokutekeleza ujenzi wa barabara hii, vinginevyo nipate... |
Hivi karibuni Serikali imetoa fedha nyingi sana kwa ajili ya kuhakikisha kwamba uchapishaji na udurufu wa nyaraka mbalimbali unaendelea vizuri. Sasa, tumetoa fedha nyingi, lakini kwa bahati mbaya Mpigachapa Mkuu wa Serikali katika eneo hili naona uzingatiaji haupo. Tunajua tuna taasisi za umma nyingi, halmashauri na ta... |
Mpaka sasa halmashauri zinaendelea kuchapisha nyaraka zake katika taasisi binafsi, wanaendelea kuchapisha mitaani na tumeshuhudia nyaraka nyingi zikiwa zinatoka nje, zinatapakaa huku na kule. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba sana kwa Mama Mheshimiwa Jenista Mhagama kwamba, hili jambo lisimamiwe kwa ukaribu, kw... |
BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Emmanuel Shangai, ajiandae Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu inayohusu bajeti ya mw... |
Tumejengewa shule za sekondari; Shule ya Sekondari Ololosokwan, Oldonyosambu, Masusu na Shule ya Msingi Loswashi iliyopo Kata ya Soitsambu. Haya ni maendeleo makubwa kwa manufaa ya Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika hizi shule, kwa jiografia ya Wilaya ya Ngorongoro wanafunzi h... |
Kila mwananchi ana haki ya kupata huduma ndani ya Tanzania. Mheshimiwa Spika, zoezi la kuhama kwa Tarafa ya Ngorongoro ni la hiari. Mheshimiwa Waziri Mkuu alienda kuzungumza na wananchi tarehe 14 Februari, 2022 na alisema ni zoezi la hiari, iweje sasa wananchi tuwawekee vikwazo vya kimaendeleo? Hata huduma za afya zime... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba wakati wa kuhitimisha Bajeti hii ya Ofisi ya Waziri Mkuu na suala hili lenyewe lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu atwambie, hawa wananchi ana mpango nao gani? Kwa sababu haiwezekani wananchi wapo miaka mitatu hawapati huduma, huduma za afya zenyewe zimekuwa hafifu. Kwa nini tuwaf... |
NAIBU SPIKA: Msiende kukaa kwenye kiti na kuzungumza na Waziri Mkuu, mnamwondoa kwenye focus ya ku-concentrate na michango ya Wabunge. Mheshimiwa Shangai endelea. (Makofi) MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa hiyo, napenda baadaye wakati wanakuja kuhitimisha hoja hii waniambie wana mpango ga... |
Wananchi hawa siyo wakimbizi, ni wananchi ambao walikuwepo. Umefika wakati ni bora wawaambie hawatakiwi kuwepo katika eneo la Tarafa ya Ngorongoro badala ya kuwapa mateso. Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine, leo kulikuwa na mradi wa elimu ambao wanafunzi walikuwa wanasomeshwa vyuo vikuu, vyuo vya kati pamoja na shul... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Rais anawaapisha viongozi pamoja na Wakuu wa Mikoa alisisitiza kwamba kila kiongozi ni lazima atende haki kwa wananchi katika maeneo wanayowahudumia, lakini pia kuondoa migogoro katika maeneo yale. Kinachoshangaza, sisi Wilaya ya Ngorongoro kwa wiki tano sasa kumekuwa na migogoro... |
Mheshimiwa Naibu Spika, amefika wilayani kwetu amewakuta wananchi wana utaratibu wao wa kujiokotea na kupata mapato yao kwenye vibanda vilivyopo pembeni mwa barabara, amewaagiza wananchi kuvunja vibanda vyao, akinamama ntile wamevunjiwa vibanda, akinamama wana mikopo kwenye VICOBA, wengine wanayo kwenye benki, lakini m... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kila mwananchi ana haki ya kulipa ushuru kwa maendeleo ya nchi lakini Mheshimiwa Rais alikataza kukusanya ushuru au kodi kwa kutumia mitutu ya bunduki. Mpaka maeneo mengine sasa hivi kumetulia na Serikali inakusanya mapato, kwa nini DC huyu aendelee kutumia mabavu na kuwaumiza wananchi?... |
(Makofi) NAIBU SPIKA: Ahsante, unaweza kumwandikia barua. Tunaendelea, Mheshimiwa Zacharia, ajiandae Mheshimiwa Kyombo. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aliyetujalia wakati huu na nafasi hii kwa rehema zake zot... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kuzungumzia suala hili la utoaji wa fedha, mtiririko wetu wa fedha siyo mzuri. Nimeipitia Taarifa ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kitengo cha Vijana tulitarajia kupeleka shilingi bilioni tatu lakini hatujapeleka hata shilingi kwenye eneo hilo la maendeleo ya vijana, hasa ... |
Barabara ya kilometa 25 kama itachukua miaka mitano, je, Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom na hatimaye Sibiti, itachukua miaka mingapi? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali, nia yetu hapa ni kwamba tupeleke huduma kwa wananchi, mkandarasi yule ameshaondoka. Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha wakae chini... |
Miradi ile tuliyosaini Jakaya Kikwete ya barabara kama saba, hakuna hata barabara moja iliyoanza mpaka leo na hali hii ni mbaya kwa sababu tumeahidi, tukasaini tena hadharani, lakini mpaka sasa hivi hakuna utekelezaji. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimelizungumza eneo hili kwa sababu changamoto kubwa ukiul... |
TAARIFA WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kumpongeza mchangiaji kwa hoja nzuri anazozitoa, lakini napenda kumpa taarifa kwa kumhakikishia kwamba, barabara hizo ambazo tulizisaini, hatujasaini na kuziacha na kazi hiyo itaanza mara moja. Kuna masuala ya kitaalam yalikuwa yanaendelea baada ya wakandarasi ... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri, amezungumza hivi punde; Juni tunapiga kura, isiwe ajabu kusema hapana kwenye kura hizi kwa sababu tunaingia kwenye ajali za kisiasa. Mimi siipokei taarifa yake kwa kweli, nitaipokea siku ya kupiga kura kwenye bajeti. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee n... |
Serikali yetu iwe Sikivu, waje na hoja. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunampenda sana, tunamwamini sana, ofisi yake ilitazame upya. Tunampenda Mheshimiwa Rais, hayuko huko na hata Mheshimiwa Waziri Mkuu ni msikivu sana. Suala hili twendeni kwa wafanyakazi tuwasikilize, wafanyakazi wanasononeka, kila unayekutana naye salamu at... |
Kama tukienda kwenye kijiji hakuna mzee wa miaka 70, wazee wote wa miaka 70 au 80 wamesharudisha namba, sisi huko tunapokwenda tunaenda na lawama kwa sababu wao wanalalamika. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli Wabunge tukianza kufikiri jambo hili ni la watu wa upinzani siyo kweli, jambo hili ni letu, tulilipitisha sisi ... |
Fursa hizi za fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu tuziongeze na fedha za miradi ya vijana tuziongeze. Tuone jinsi ya kuwatafutia vijana wale madirisha ambayo baadaye wataona Serikali imewajali. Changamoto ya ukosefu wa ajira ni dunia nzima wala siyo Tanzania na kwa sababu hiyo, basi kila nchi inapambana na hali yake kuona kw... |
Samia Suluhu Hassan na tunaona pongezi hizi zinakwenda kwa sababu taarifa iliyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, inaonesha dhahiri kwamba Mheshimiwa Rais wetu amedhamiria na ni mbeba maono wa nchi yetu na anamaanisha anachokisema. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, mahususi nimpongeze sana Mheshimiwa Kassim Majaliwa ... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nitaangalia katika eneo la utawala wa sheria, ambalo katika taarifa ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, limeelezwa kuanzia ukurasa wa 24. Tunaona Serikali imeboresha kabisa Mahakama zetu, tumejengewa vituo jumuishi vya kisheria, vituo jumuishi vya haki, lakini tunaona Mahakama za Rufaa za Mikoa,... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, suala langu la pili nitaenda kwenye Sekta ya Uzalishaji, ambalo katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ameielezea kuanzia ukurasa wa 26 na kuendelea. Niipongeze Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha wakulima kupata mbegu bora, mbolea, zana bora za kilimo na za kisasa na... |
Zao hili limesaidia hasa katika kuongeza thamani ya mashamba yetu ya ndizi ambapo migomba ilikumbwa na ugonjwa mnyauko, lakini baada ya kuingiza zao la vanila, ukichanganya na zao la Kahawa tumeanza kupata angalau kipato na kumwinua mwananchi. Mheshimiwa Naibu Spika, nisikitike kusema kwamba Serikali imekuwa kimya kati... |
Kwa imani tuliyonayo naamini ukimya wake atakuja na mkakati wa kishindo kwa zao hili la vanila. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama Mtendaji Mkuu wa Serikali, lakini pia mlezi wa Mkoa wa Kagera. Kama ni mlezi, tunatamani aje na neno ambalo atasema juu ya vanila za Mkoa wa Kagera. Tunapotaka kujikwamua kiuchumi ni kwa sababu G... |
Kwa hiyo, niombe sana kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika eneo hili kama Wanakagera wanataka kuona mkakati mahususi ambao una-reflection katika bajeti, ni zao letu la vanila katika maeneo manne. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kwanza, zao hilo litambulike; suala la pili, kutafuta soko la uhakika la ndani na nj... |
Mheshimiwa Naibu Spika, niupongeze uongozi wa Mkoa wa Kagera chini ya Mheshimiwa Hajati Fatuma Mwasa na Mheshimiwa Mkuu wetu wa Wilaya Kanali Hamisi Maiga lakini na Mkurugenzi wetu wa Halmashauri Advocate Paul Wanga na wasaidizi wake, pamoja nami kama mwakilishi wa wananchi na Waheshimiwa Madiwani, tumekuwa tukishiriki... |
Mheshimiwa Naibu Spika, wapo wanunuzi wachache wachache ambao wananunua mazao hayo, lakini inaonekana wameelemewa kwa sababu nao katika soko la dunia, wapo kama Tanzania, hawaoni kama kule nje tuna soko. Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tatu, nitaongelea kwenye maliasili, ambalo imeelezewa vizuri katika ukurasa wa 34 w... |
Wakati Mheshimiwa Rais anarekodi hii rekodi ya Royal Tour alikuwa katika mbuga ambazo zina risk kubwa, lakini kwa sababu ya uzalendo na upendo kwa nchi yake aliona afanye hiyo kazi yeye mwenyewe ili iweze kuleta impact ambayo leo tunaiona. Tumpongeze Mheshimiwa Rais kwa uzalendo na utashi na maono yake kuyasimamia kwa ... |
Leo katika Wilaya ya Missenyi tuna uvamizi mkubwa wa tembo katika maeneo ya Missenyi Ranch pamoja na wananchi wa Mabale wote na hata kilimo kimesimama. Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia wanaharibu mali za wananchi, hawawezi kuvuna mazao, lakini pia wananchi wanajeruhiwa, pia tunaona miundombinu yote inayojengwa kwa m... |
KYOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Asya Sharifu Omar, wajiandae Mheshimiwa Esther Matiko na Mheshimiwa Mariam Nyoka. MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi asubuhi hii ya leo ya kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri... |
Tumeguswa sana na jambo hili. Kwa hiyo nimeona nilichangie hili kutokana na wimbi kubwa la ukatili unaoendelea siku hadi siku. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu Serikali yetu namna inavyoendelea kupambana na haipendezwi na vitendo hivi vinavyofanywa na wachache ambao wanajifanya wamejizima data, jambo hili ha... |
Kwa hiyo sasa, niiombe Serikali ione haja ya kuibadilisha sheria hii na kuwekea adhabu ya kuwahasi hawa wote ambao wanafanya vitendo hivi kwa makusudi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, matukio haya ni mengi sana na kwa kweli Watanzania yanatuumiza tukiwemo wanawake, tunashuhudia vitoto vichanga vinatiwa kwenye maji, vi... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, nasema haya kwa machungu makubwa kama mwanamke, kama mama, kama mzazi, inauma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapambana usiku na mchana, tukijipima sisi na yeye, bora sisi tunapumzika, tunakaa kuliko yeye anavyohangaika kututafutia maisha bora, inakuwaje wanatokea watu wachach... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niondoke kwenye udhalilishaji niingie kidogo kwenye suala la maji, kwa sababu suala la maji linatugusa na ni suala la kila siku. Katika suala hili la maji nizungumzie Sera ya Maji. Hii lengo lake ikifika 2025, mijini ifikie 95%, lakini vijijini 85%. Suala hili ni kubwa na tunaipong... |
Jambo hili litaleta afya, kwa sababu inapokwenda miradi kama wanajamii hawashirikishwi inaleta manung’uniko na tija ya Serikali itakuwa haipatikani. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, ndoto ya Mama Samia ni kubwa katika kumtua mama ndoo kichwani. Tuseme ukweli, tunamshukuru sana Mama Samia, ameweza kututua ndoo kichwani ... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, maji ndiyo kila kitu, lakini Serikali inapopeleka miradi katika maeneo ya wananchi, kuna vyanzo vya maji ambavyo vingine havizingatii kuweka maeneo ya malisho kwa wafugaji, jambo linalopelekea vyanzo hivyo kuharibiwa wakati Serikali tayari imeshawekeza pesa nyingi pale. Sasa ikiwa maji ... |
Naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa maeneo mawili, kwanza ni kwa kudumisha demokrasia na kuimarisha demokrasia nchini. Sasa hivi tunaona hata sisi wapinzani tunafanya mikutano ya ndani, tunafanya mikutano ya hadhara, tunafanya maandamano kwa amani ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo tulikuwa hatuwezi kufanya miku... |
Kwa mfano, tulipokuwa tunafanya uchaguzi na Mheshimiwa Spika wetu alikuwa anagombea Urais wa Umoja wa Mabunge ya Dunia, kwa kweli tulikuwa tunapata ushirikiano mzuri sana kwa Mataifa mbalimbali na ndiyo maana hata tukaweza kuibuka. Hii yote imechagizwa na jinsi mama anavyoji-position na Mataifa haya ukilinganisha na hu... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, alikuwa na ziara Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 mpaka tarehe 29, alishuhudia kero mbalimbali, lakini kwa masikitiko, baadhi ya hizo kero zimeendelea hata baada ya ziara yake. Nitazungumzia madhila ambayo tunayapata wananchi ambao tunazunguka Mbu... |
Huyu kijana mpaka tunavyoongea hajapatikana akiwa hai wala akiwa amekufa ili wamrudishe tuweze kumhifadhi kwa mila na desturi za Wakurya. Hilo limetokea tarehe 21 Machi mwaka huu 2024. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tukio lingine ambalo lilitokea Agosti mwaka 2023, kijana Julius Mwita Mmali wa Kijiji cha Kenyams... |
Haya yanaondoa na ku-tarnish the government. Tunataka uhai wa watu wanaoishi... NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa. MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye hizi mbuga, huwezi ukathamini mbuga vis-a-vis uhai wa binadamu ambao wanazunguka hizi mbuga. (Makofi) NAIBU WAZIRI W... |
Kilichobainika ni kwamba, hakuna ushahidi wa wazi kwamba jambo hili lilihusisha Askari wetu. Damu iliyoonekana kwenye eneo la tukio ilipelekwa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Matokeo yake yanasema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba damu hii ni ya binadamu. Mheshimiwa Naibu Spika, linapokuja suala la maisha ya ... |
ESTHER N. MATIKO: (Hapa alizungumza bila kutumia kipaza sauti). NAIBU SPIKA: Unabishana na kiti sasa? (Kicheko) MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaongea kwa nia njema kabisa kuhakikisha Serikali inasimamia uhai wa Watanzania. Ninachokiongea, kuna series za events za mauji kwenye hifadhi na hili likiwepo... |
Wanasema hilo eneo, wanawapiga risasi wanaanguka na kuna mamba wanakula hao binadamu. Ukiona kwenye hilo eneo kuna nguo nyingi. Waziri anajua, Katibu Mkuu wa Wizara anajua nimewapelekea. Sasa hivi ni miezi mitatu no action, nothing! Hatuwezi kukubali hii laana, mbuga kugeuka kuwa laana badala ya kuwa neema kwenye nchi ... |
Mwaka 2013 nilikuwa Mbunge hapa, ilitokea dhuluma hii hii tukalalamika, kulikuwa na Operesheni Tokomeza, ikaundwa Kamati Teule ya Bunge ikaenda ikagundua madudu na zaidi ya Mawaziri watano waliwajibika. Tunaongea siyo kisiasa, tunaongea bitterly. Mama ana dhamira ya dhati, our people wanauawa. Msiweke huu utani kwa mai... |
(Makofi) (Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) NAIBU SPIKA: Ahsante. Kengele ya pili hiyo. Mheshimiwa Nyoka atafuatiwa na Mheshimiwa Toufiq. (Makofi) MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu. Awali ya yote, naomb... |
Kiasi cha mikopo hiyo kwanza ni kidogo ukilinganisha na mikoa yote ya Tanzania kwamba ipate mkopo wa shilingi bilioni moja kwa vijana wote, hii siyo sawa. Pamoja na changamoto ya kiasi hiki kuwa kidogo, uelewa wa vijana wetu kule vijijini juu ya mikopo hii, ni mdogo. Tunawaomba wataalamu wetu waende vijijini wakatoe el... |
Nawaomba wataalamu wa NIDA waende vijijini wakawasajili vijana hawa, kwa kuwa mara ya mwisho kwenda vijijini ilikuwa ni mwaka 2016. Hata walivyoenda kwenye vijiji hivyo, wamewasajili lakini changamoto kubwa ni katika upelekaji wa vitambulisho hivi. Mheshimiwa Naibu Spika, vitambulisho hivi wengi wao wamepata namba tu, ... |
Mpaka hivi ninavyoongea, tathmini tatu zimefanyika juu ya barabara ile, lakini majibu ya Serikali yamekuwa mchakato unaendelea, pia barabara hii imeunganishwa na Barabara ya Lutukila, siyo kweli. Kwani barabara hii ikitengenezwa, wananchi wale wakafurahia na Serikali yao si itakuwa inafurahi wananchi wao tukiwaondolea ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naiomba Serikali, kati ya mambo yote muhimu inayoyafanya, tuuangalie Mkoa wa Ruvuma kwenye hii changamoto kubwa inayopatikana pale, juu ya suala zima la barabara ya by pass inayotoka Mletele kuelekea Namanditi. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, pia naipongeza Serikali ka... |
Tunaomba wakanufaike badala ya kundi la watu wachache wananufaika na mikopo hii. Wananchi wetu, wale vijana wetu hawafahamu hii, wanafahamu zaidi ile ya asilimia 10 tu ya halmashauri. Kwa hiyo, naomba Serikali ifanye utaratibu mzuri, ifanye maandalizi mazuri, namna ya kuwafikia vijana wetu wa nchi nzima ili nao waweze ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, nami pia naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge wote ambao wameshachangia kwa kuendelea kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuhakikisha kwamba Watanzania tunapata maendeleo endelevu. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wa miradi ya kielelezo ambayo ipo miradi minane, nitazungumzia ule mradi wa uwekezaji wa kiwanda cha Mkulazi ambacho ni kiwanda cha sukari. Kiwanda hiki kimewekezwa kwa pesa ya ndani kwa asilimia 100. Naomba niipongeze sana Serikali kwa kuweza kuwekeza katika kiwanda hiki. Pia... |
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaamini kwamba iwapo kiwanda hiki uzalishaji wake utafikia ile full swing ambayo ni tani 50,000 kwa mwaka, itasaidia kupunguza ile nakisi ya sukari ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara nchini, lakini ninaamini kabisa kwamba kama mradi huu utatekelezwa vizuri, maana yake uzalishaji unaweza uka... |
Sasa je, Serikali haioni kwamba umefikia wakati wa kuangalia namna bora kwamba pengine kama imebainika kuna majanga kama hizo mvua za El-Nino ambazo zinaweza zikaleta athari, yale matenki ambayo yapo pale, ule mchuzi unaozalishwa kwa kukamua ile miwa uweze kupatikana kwa wingi zaidi ili kusudi mchuzi ule uweze kuhifadh... |
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nilitamani kulizungumzia ni kuhusiana na masuala ya wafayakazi ambayo ipo ukurasa wa 74 hadi ukurasa wa 83. Naendelea kuipongeza sana Serikali kwa kuratibu uzalishaji wa fursa za ajira ili Watanzania hasa vijana ambao ni kundi kubwa sana, ambao wamekuwa na tatizo kubwa sana ... |
Vijana wenye ulemavu wamekuwa wakipata stadi za ujuzi kama ufundi cherehani, ufundi magari, ufundi uashi, ufundi bomba na mengineyo mengi. Kwa hiyo, hii ya ujuzi ina maana kwamba mwisho wa siku vijana hawa wote wenye ulemavu na ambao wapo kawaida wataweza kujiajiri wao wenyewe na hatimaye waweze kujikwamua katika suala... |
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuishauri Serikali kwamba ni budi ikafanya shopping katika zile nchi nyingine ambazo bado zina upungufu sana wa ajira ili kusudi Watanzania pia waende katika nchi nyingine ikiwemo pengine Canada, Switzerland na nchi nyinginezo ambazo pia kuna nafasi za ajira ili kusudi vijana w... |
Mheshimiwa Naibu Spika, nikitaja nchi chache miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Egypt ambayo imeweza kupata dola bilioni 24.5, lakini pia wenzetu Nigeria wameweza kupata dola bilioni 20.5, Morocco wameweza kupata dola bilioni 12.1, Ghana wameweza kupata dola bilioni 4.9, Kenya pia wenzetu nchi jirani wameweza kupata d... |
(Makofi) MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia katika Wizara hii muhimu sana. Kuna msemo unaosema; “progress is a double edge sword” au maendeleo ni upanga wenye makali kuwili, ikiwa na maana kwamba kwa namna yoyote tunayopata maendeleo kuna hasara fulani fulani zina... |
Pia tumeona Mheshimiwa Rais anapiga kelele kuhakikisha kwamba asilimia kumi za vijana zinarudishwa tena kwa utaratibu ulio bora. Hii yote ni kumkomboa kijana wa kawaida. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, katika hili nina machache ya kushauri. Moja, pamoja na kwamba tunapigia kelele zaidi asilimia kumi ambazo kaka yangu ... |
Fedha hizi zilikuwa zinatusaidia sana, tunaomba mzirudishe ili ziendelee kutusaidia. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia nilikuwa nashauri kitu kimoja. Bunge hili katika utashi huu huu wa kumkomboa kijana wa Kitanzania, mwaka 2023 tulipitisha Sheria ya Manunuzi. Katika sheria hii tuliandika kwamba 30% ya fedha zote za... |
Ninaamini tatizo la vijana kukosa ajira changamoto hiyo inaenda kwisha tukihakikisha fedha hizi zinakwenda zinapotakiwa. Tunaomba sana Serikali iliangalie. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia niliwahi kushauri katika Bunge hili Tukufu kwamba kulikuwa na program ya NSSF kwa vijana. Nikiwa Mjumbe wa Kamati ya Katiba na ... |
Namshukuru sana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mheshimiwa Jenista, alipokea wazo hili na akasema wanakwenda kulifanyia kazi ili vijana wa vyuo na vyuo vikuu wakiwa wanajiwekea akiba ndogo ndogo kupitia fedha zao za kujikimu na mikopo wanayopewa na Serikali by the end of three to four year... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia tuna Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ulio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nchi hii inaongoza kwa mipango. Katika Mpango wa Miaka wa Miaka Mitano tuliopitisha ndani ya Bunge hili tukiwa tunaanza mwaka wa kwanza, tulipisha kwamba mfuko huu kwa miaka yote mitano utapewa kiasi cha shilingi ... |
Mheshimiwa Naibu Spika, maombi yanayotolewa katika mfuko huu ya vijana kuhitaji mikopo ni mingi, lakini badala ya kutafuta vyanzo vingine kuongeza fedha katika mfuko huu kufidia fedha ambazo zimekuwa hazitolewi kwa miaka mingine, badala yake wanapunguza zaidi fedha hizi. Katika hili naomba Mheshimiwa Waziri anapokuja k... |
Utaratibu huu kwa sasa siyo formal, naiomba Serikali ije na sera ambayo itaruhusu na ikiwezekana kulazimisha taasisi mbalimbali za Serikali kuwapokea vijana wanaojitolea ili waweze kupata uzoefu, lakini pia katika kujitolea huko wanachangia katika pato la Taifa. Pia kijana akiruhusiwa kujitolea katika sekta hizi za Ser... |
Tuombe Serikali ije na sera ambayo italazimisha vijana kukubaliwa kujitolea kwenye sekta mbalimbali. Mheshimiwa Naibu Spika, niliwahi kuliulizia nikaambiwa kwamba changamoto ni kwamba vijana wanaonekana watavujisha siri. Nadhani ni jukumu la Serikali kuhakikisha kwamba inatunza taarifa zake ili ambaye hatakiwi kuziona ... |
Pia namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi njema anayoifanya hasa katika majimbo yetu na miradi ya maendeleo ambayo kimsingi tumeshuhudia katika maeneo yetu ya majimbo. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kweli anafanya kazi nzuri ambayo Wabunge na wananchi wanaiona. Mheshimiwa Wazi... |
Ukigawa hiyo idadi ya vijiji, unaweza kukuta kila jimbo lina kijiji kimoja, lakini mimi kwangu viko 19 ambavyo havijawaka. Naomba tu kwa kweli, najua Mheshimiwa anafanya kazi kubwa, basi iwekwe nguvu kidogo kwa yule mkandarasi amalize vile vijiji. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua kuna mradi unaokuja unaoitwa Uj... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika maeneo ya utawala, Mheshimiwa Waziri Mkuu, ukiangalia sensa iliyopita ya mwaka 2012, tulikuwa Watanzania kama milioni 40 na kitu, leo tuko milioni 61. Sasa maeneo ya utawala kwa kweli kule yamekuwa makubwa, hasa kwenye Jimbo la Mbulu Vijiji na maeneo mengi. Vijiji na kata zin... |
KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba wachangiaji waelekeze hoja kwenye Kiti. Hii kuwatajataja Mawaziri na kumtaja Mheshimiwa Waziri Mkuu, anamtoa kwenye reli. Ana document pale anasoma, lakini kila saa anasikia Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, yeye anatakiwa aongee na kiti. Naomba ungewaelekeza wachangiaji namna hiyo. (Mak... |
Ukiangalia kwenye folder la maendeleo tuliyotengea shilingi bilioni 482.2, ukiangalia mpaka sasa hivi wamepewa shilingi bilioni 280.2. Ukiangalia, ni wazi kwamba kutokana na fedha zilizotolewa, siyo rahisi miradi yote ikatekelezwa. Ukiangalia sasa hivi, wakandarasi wengi wako site na hawana namna yoyote kwa sababu hawa... |
Kutokana na bajeti hapa, nimeangalia kwenye bajeti hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu hasa kwenye upande wa maafa, hali siyo njema. Ukiangalia pale Hanang tulipeleka fedha nyingi na tunashukuru sana Watanzania wengi waliweza kuchangia, lakini sisi kama Serikali tungetenga bajeti kubwa hapa ingekuwa rahisi kusaidia Wizara ya... |
Maana yake ni kwamba wananchi watajua hii tumeshawadanganya, lakini ili tusionekane waongo, ni vizuri zaidi tukapeleka fedha, wakandarasi wakaendelea. Maana yake, ukiangalia kitaalam hapa, kama barabara imesainiwa mwaka 2023 na tunaendelea kukaa hivi tu, maana yake ni kwamba gharama itapanda na kama barabara ilikuwa in... |
Uko ndugu yangu Mheshimiwa Ndejembi, Mheshimiwa Ummy na Mheshimiwa Katambi uko hapo. Hebu saidieni vijana katika nchi hii, mikopo hii inatakiwa na vijana. Tumeshapata maswali mengi kule. Najua utaratibu haukuwa mzuri, basi wekeni utaratibu wa kibenki vizuri kabisa vijana wapate mikopo. Nina uhakika vijana wakipata miko... |
MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Awali ya yote, naomba nichukue nafasi hii nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya uhai na nimepata muda wa kuchangia hotuba hii. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nichukue nafasi hii nimsh... |
Namshukuru na kumpongeza pia ndugu yangu, rafiki yangu Mheshimiwa Deo Ndejembi kwa jinsi anavyoisaidia Serikali katika kutekeleza majukumu mbalimbali. Vilevile nawapongeza Waheshimiwa Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kwa kumsidia Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kutekeleza majukumu yake mbalimbali. (... |
Naomba Serikali kwenye suala hili la mapato iendelee kupanua wigo wa vyanzo mbalimbali vya mapato ili tuweze kuongeza mapato yetu, yaweze kutusaidia katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwenye suala la miundombinu ya barabara. Mwanzo kabisa katika Jimbo langu nilikuwa napat... |
Sehemu hiyo ilikuwa imeharibika sana na wananchi wa kutoka eneo la Mpepai walishindwa kusafirisha mazao na hata kusafiri katika hali ya kawaida kuja eneo la Mbinga kwa ajili ya kumaliza shughuli zao mbalimbali za kijamii. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia kulikuwa na changamoto ya barabara ya kutoka Mbinga – Kikolo ... |
Mradi huu utasaidia kutengeneza barabara za pale Mbinga Mjini pamoja na miradi mingine ambayo itaisaidia halmashauri kuongeza mapato mbalimbali. Kwa hiyo, naiomba Serikali isimamie na itekeleze mapema mradi huu wa TACTIC. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, pia, naipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji... |
Pili, imejenga majengo mengi katika shule mbalimbali ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wetu wanapata elimu katika mazingira mazuri. Pia, Serikali inaendelea kutoa mikopo ya elimu ya kati pamoja na elimu ya juu. Naipongeza sana Serikali. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuimarisha miundombinu kwenye shule zetu za ... |
Baadhi ya maeneo hayo, Serikali tayari imeanza kupeleka nguzo. Tunategemea baada ya mvua kufika mwisho, Serikali itakamilisha miradi hiyo na itaendelea kupeleka maeneo mbalimbali. Naomba kushauri kwamba mara baada ya ukamilishaji wa upelekaji wa miradi ya umeme kwenye vijiji, naomba Serikali ianze kupeleka umeme kwenye... |
(Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali vilevile kwani tulipewa shilingi milioni 900 kwa ajili ya kukarabati hospitali kongwe. Kazi hiyo imeanza na wananchi wale wamefurahi sana, lakini naomba tuongezewe fedha ili tuweze kukamilisha ukarabati na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga. (Makofi)... |
Hii ni barabara kuu namba nane, wahandisi waliita T8 (Trunk Road No. 8) katika nchi hii, na ilipitishwa tangu mwaka 1980, na ilianza kujengwa tangu mwaka 1984 pale Mwanza. Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka leo hii nasimama hapa Bungeni, barabara hii haijakamilika kujengwa tangu mwaka 1984 mpaka leo, na kipande ambacho haki... |
Samia Suluhu Hassan, alipokuwa Singida alitoa agizo kwa Wizara ya Ujenzi kwamba wafanye mbinu zozote, mikakati yoyote iwayo ili waweze kuijenga barabara hii na ikamilike kwa ukamilifu wake, kwa maana ya barabara hii ya Trunk Road Number 08 pamoja na vipande vyake viwili. Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma sana Ilani zetu... |
Mheshimiwa Naibu Spika, Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005 ilitaja pia, Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ilitaja pia, Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ikataja tena, Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 ikataja tena, lakini mpaka leo hii nasimama hapa Bungeni utekelezaji bado haujakamilika. Mheshimiwa Naibu Spika, kutojengwa kwa ... |
Usafiri na usafirishaji wa bidhaa umekuwa wa gharama kubwa kwa sababu barabara hii haijajengwa na wakati wa mvua inakuwa inakatikakatika. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano mwaka huu, barabara hii katika eneo la Ipemba - Mpazi ilikatika vipande vinne, maeneo manne yalikatika kabisa, na kwa hiyo, hakukuwa na usafiri kati... |
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ni kengele ya kwanza. Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 22 Oktoba, 2008 Rais Kikwete alitembelea barabara hii, alitaka kwenda Kitunda akakwama njiani kwenye tope kwa sababu ya barabara hii kutojengwa. Akaagi... |
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu ambalo napenda kuzungumzia, sisi tuna mradi wa kilimo cha umwagilia pale Sikonge katika Bwawa la Uluwa. Bwawa hili la Uluwa lilichimbwa kama utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kilimo cha Umwagiliaji Maji Mashamba uliokuwa unatekelezwa mwaka 1975 baada ya Azimio la Iringa la Halmashau... |
Mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2006/2007 kwa Serikali kutoa zaidi ya shilingi bilioni 379. baada ya mradi kuanza, ulipoonekana kwamba unachota kama hekta 500 kutoka kwenye eneo la hifadhi ambalo ni hifadhi ya Halmashauri, watu wa maliasili wakauzuia huu mradi. Serikali imeingia gharama, lakini watu wa maliasili wa... |
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba sana kupitia Bunge lako hili Tukufu, Serikali hasa Wizara mbili; Wizara ya Kilimo na Wizara ya Maliasili, wakae pamoja, waje Sikonge, waturuhusu tuweze kutumia huu mradi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wetu. Ilikuwa ni hayo tu. Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja ya Wazi... |
Kama Serikali, wote tunafahamu kwamba Serikali ya Awamu ya Sita tangu imeingia madarakani suala la haki jinai, ili kuhakikisha Watanzania wanakuwa salama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amelipa kipaumbele kikubwa sana. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, ka... |
Hivyo basi, Bunge hili liwe limemtendea haki Mbunge na pia liwe limeitendea haki pia Serikali. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba Mwongozo wako. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Chief Whip, ahsante. Ni kweli Mheshimiwa Rais aliunda Tume ya Haki Jinai na Tume hii ilipewa muda, wakaomba waongezewe na Rais akakubal... |
(Makofi) Madhumuni ya kuweka tume hii ni kubainisha changamoto na vilevile kuwachukulia hatua watu ambao wanaharibu jina la Rais na jina la Serikali kwa masilahi yao kama hizo tuhuma zitakuwa ni za ukweli. Kwa hiyo, nakala zimekuja mbili, moja itakabidhiwa Serikali na moja itabaki katika Ofisi ya Spika kwa kazi za Kibu... |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.