text
string
Kanuni ya Saba ya Kanuni za Bunge imeelezea uwepo wa wenyeviti watatu wa Bunge ambao huongoza vikao kwa utaratibu na maelekezo ya Spika au Naibu Spika na Kanuni za Bunge. Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 13(2) imeelezea nyakati mbalimbali ambapo uchaguzi unaweza kufanyika, mojawapo ikiwa ni mara baada ya Kiti cha Mwenyek...
Waheshimiwa Wabunge, kutokana na nafasi mbili za wenyeviti kuwa wazi na msingi wa masharti ya Kanuni ya 13 na taratibu zetu, siku ya Ijumaa tarehe 5 Aprili, 2024 Kamati ya Uongozi ilikutana na kwa kauli moja ilipendekeza majina mawili ya Wabunge wenzetu yawasilishwe Bungeni ili wathibitishwe kuwa Wenyeviti wa Bunge. Ma...
(Makofi) Utaratibu kama huu ulitumika kwenye uchaguzi wa Wenyeviti Wabunge katika Bunge la Kumi, Bunge la Kumi na Moja, na Bunge hili la Kumi na Mbili linaloendelea ambapo Kamati ya Uongozi ilipendekeza majina yanayolingana na nafasi zinazogombewa na baadaye majina hayo yalithibitishwa na Bunge. Waheshimiwa Wabunge, kw...
Baada ya kuwahoji, sasa hayo ndiyo maamuzi ya Bunge, leo tumewachagua ndugu zetu hawa wawili, Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama na Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika kuwa Wenyeviti wa Bunge. Mimi na Mheshimiwa Naibu Spika tunawakaribisha kwenye safu ya Uongozi wa Bunge. (Makofi) Waheshimiwa Wa...
(Makofi) Mheshimiwa Spika, nitoe ahadi kwamba nitajitahidi kwa kadri nitakavyojaaliwa na Mwenyezi Mungu kutekeleza jukumu hili muhimu sana kwa heshima ya Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa heshima ya Taifa letu. Ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika. MHE. DEOD...
Kwa namna ya pekee, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili kwa namna ambavyo wameonesha hapa kwamba wana imani kubwa nami katika kushika nafasi hii ya kuliongoza Bunge katika kumsaidia Spika na Naibu Spika. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nitoe ahadi kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwamba nitaifanya kazi hii kwa we...
Wageni wangu saba ambao wanatoka Kampuni ya Bima ya UAP Insurance Tanzania, ambao wapo viwanja vya Bunge kwa ajili ya kutoa elimu ya Bima kwa Waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi wa Bunge, wako pamoja nasi hapa Bungeni. Karibuni sana. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, maonesho ya Kampuni hii yako nyuma ya Ukumbi wa Ms...
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa nimepata nafasi hii ya kwanza kuchangia, nichukue nafasi hii kukupongeza sana, tuna imani na wewe, chapa kazi, najua unaweza. Kipekee kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Katika miaka mitatu ya uongozi wake tumeona kazi ...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania kazi kubwa imefanyika, Mheshimiwa Rais tayari amelipa kiasi cha shilingi bilioni 753, ndege tatu zilizoagizwa, tayari mbili zimefika, moja itafika mwezi huu. Sasa tunakuwa na ndege 16 katika Shirika letu la Ndege la Tanzania. Kazi inaendele...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zilizofanyika ni nyingi sana, hata nikisema hapa nitandelea kusema kwa muda mrefu, lakini nashukuru hata wenzangu wamechangia na kusema ni namna gani Mama yetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo. Mheshimiwa Mw...
Katika changamoto hizo, ya kwanza ninayoweza kwenda kuisemea siku ya leo ni changamoto ya mbegu bora au miche bora. Hii imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wakulima wetu. Kwa kuwa hawapati mbegu bora au hiyo miche bora, wanaenda kufanya kilimo ambacho kinakuwa hakina mazao yanayokidhi vigezo, wanakosa thamani kubwa au...
Nilikuwa nashauri, Serikali sasa ifuatilie kwenye suala la kilimo cha umwagiliaji, waweke mabwawa ya kutosha. Mvua zinanyesha na kuleta athari kwa wananchi na wakati mingine mpaka mafuriko. Kwa nini basi Serikali isione namna ya kutumia maji haya kwenda kwenye kilimo cha umwagiliaji na wananchi wetu wakaweza kupata fai...
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kusema jambo lingine ambalo linawakwamisha wananchi au wakulima wa Kilimanjaro ambalo ni soko la ndani na nje. Bado tumekuwa na shida kubwa sana ya kupata masoko kwa ajili ya bidhaa zetu. Kama ndizi zetu akina mama wa Kilimanjaro tunataka kuona zinaenda nje ya nchi, zisiishie kupelekwa...
Wakulima hawa wana mashamba kiasi gani? Je, kama tunahitaji mbolea, pembejeo na miche, wanawezaje kujua kama hawajui idadi ya hawa wakulima? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali iangalie ni namna gani itapata takwimu sahihi za wakulima wa kahawa, wakulima wa ndizi, wakulima wa parachichi, wakulima wa maua...
Tunajua Serikali inafanya mikakati na mipango ya kuweza kuboresha, lakini basi waweze kupewa taarifa ni lini fedha hiyo inatoka na Serikali itoe tamko ili akina mama wa Kilimanjaro nao waweze kufaidika. Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, naunga mkono hoja. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther Malleko, ahsante sana. Sa...
Namshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya wananchi wa Mbogwe, kweli kabisa Mbogwe sasa hivi inaanza kuonekana kwenye ramani ya dunia, mwanzoni ilikuwa haionekani. Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa sababu zipo barabara ambazo zilikuwa hazipitiki kabisa, lakini kwa sasa zimeanza kupitika. Pa...
Kwa hiyo, ili Serikali ilione la maana sana kuweza kuliondoa, Serikali ifanye mambo yake yenyewe tu na wananchi waweze sasa kustarehe. Mheshimiwa Mwenyekiti, inakuwa ni karaha ambapo miradi inakuja kijijini halafu mnaanza kuambiwa kusomba mawe, kusomba matofali halafu unakuta pesa zimetolewa shilingi milioni 450. Kiuha...
Naiomba sana Serikali, kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mdogo mwaka 2024/2025, iende ikayaezeke haya maboma kwa sababu wananchi waliumia, waliuza kuku wengine wakajenga haya maboma. Sera ya Serikali ilikuja ili kila Kijiji kiwe na zahanati na wananchi wakajitahidi wakafanya hayo mambo. Kwa hiyo, naiomba sana Serikali ...
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninaloliomba hapa kwenye Wilaya ya Mbogwe, miradi ya Serikali kutokukamilika kwa wakati. Mwanzoni wakandarasi walikuwa wakifanya kazi, shughuli zilikuwa nzuri, shughuli zilikuwa na ubora. Hizi force account miradi inasimamiwa na wataalam, ni kelele tupu. Tumemwona hapa Mheshimiwa Wa...
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tungerudi kwenye miaka ile ya nyuma jinsi walivyokuwa wakitengeneza wakandarasi, ambapo miradi ilikuwa inatengenezwa yenye uimara kuliko ilivyo hivi sasa, kila sehemu ni kelele. Wataalam wanakula fedha, mainjinia wanakula fedha, tunakalia kugombana na kutokufanya shughuli nyingine. Mhes...
Kwa hiyo, Serikali ione kila namna kuvitofautisha vikao ili wakati wa Bunge uwe wa Bunge tu, ili wakati wa Baraza la Halmashauri kule Waheshimiwa Wabunge tuweze kushiriki ili hata wananchi wanapotuhukumu, watuhukumu katika kweli. Sasa hivi mambo mengi yanafanyika Wabunge hawapo kwenye majimbo yao, matokeo yake ni kupat...
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, nizungumze kidogo kwa vile huu ni mwaka wa uchaguzi, tumepitisha hapa Sheria ya Vyama vya Siasa pamoja na mambo mengine. Namwombea Mheshimiwa Rais, kwa roho yake ya upendo kabisa, aendelee kusimama na Mungu hivyo hivyo. Nami nasema, tuko tayari kwa mapambano 2024/2025, afe kipa afe...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) MWENYEKITI: Mheshimiwa hitimisha hoja yako, uko nje ya muda. MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nahitimisha hoja yangu kwa kumwombea Mheshimiwa Rais ili haki itendeke 2024/2025 na kazi iendelee. Ahsante sana. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana...
Tunaamini uzoefu wako kwenye mambo ya sheria na uzoefu wako wa kibinadamu wa mahusiano yako na Wabunge wenzako utakuwa ni chachu ya kuweza kumsaidia Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti wenzako katika kuongoza shughuli za Bunge. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa W...
Wako watu wanaona wivu, ni kwa nini tunampongeza? Kwa uhalisia sisi tulioko ndani ndio tunajua ni yapi Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyafanya kwa Watanzania katika majimbo yetu na wananchi wetu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la elimu, kule jimboni kwangu mambo ni mazuri. Tuna shule ya vipaj...
Mfano, Morogoro tuna Hifadhi ya Mwalimu Nyerere, Mikumi na Udizungwa, ukienda Iringa kuna Ruaha, ukienda Katavi kuna Hifadhi ya Katavi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nina taarifa fupi kwamba kupitia Hifadhi ya Mwalimu Nyerere, mwaka 2022/2023 kulikuwa na wageni karibu 34,189 wa kutoka nje ambao walifika kufanya utali...
Ninakumbuka katika bajeti iliyopita nilipiga kelele kwenye hili, ujenzi wa uwanja wa ndege, lakini kupitia Mradi wa E- Grow safari hii uwanja wa ndege umejengwa kwenye lango la kutokea Matemere. Vilevile, kuna ujenzi wa campsite yenye uwezo wa watu 100, rest house yenye uwezo wa kulaza wageni 20, vilevile kuna ujenzi w...
Samia Suluhu Hassan, kwa kujua umuhimu wa utalii kwenye Nyanda za Kusini, na hasa Hifadhi ya Mwalimu Nyerere, ameweza kuidhinisha kujengwa kwa kiwango cha lami kilometa 78. Hiki ni kichocheo cha kutaka tupate watalii wengi na tupate fedha nyingi za kigeni ili tuweze kuendeleza uchumi wetu. Mheshimiwa Mwenyekiti, lingin...
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali, kupitia zao hili kama Taifa upande wa Tanzania Bara, na lenyewe linaweza likaleta fedha nyingi za kigeni ambazo zitaingia kwenye shughuli za kuleta maendeleo kwa Taifa letu. Naiomba Wizara isimame, iungane na viongozi wa Mkoa ili ikiwezakana zao la karafuu nalo litangazwe...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) MWENYEKITI: Mheshimiwa, hitimisha hoja yako, ahsante. MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Naomba kuunga mkono hoja. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Innocent. Anafuata Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri, Mheshimiwa ...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo, nitaanza kuchangia mchango wangu katika Sekta ya Maliasili na Utalii. Kwanza naipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii, Watanzania wote tunaona jitihada ambazo mama anazifanya na jinsi ambavyo sasa hivi watalii wameongezeka katika Taifa letu na kuongezeka kwa fedha ...
Imefika mahali sasa nyani wale ambao wako katika msitu wetu wa TANAPA, KINAPA pamoja na TSF wanakuja mpaka maeneo ya nyumba za watu na hata wakati mwingine wakikosa kitu cha kula wanachukua watoto wadogo. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la kusikitisha kwa sababu, hili lilitokea Rombo na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo alifa...
Wananchi waliokuwepo walikimbizana wakaenda kutafuta ndizi, walipopata ndizi wakarusha kule chini bondeni walikokuwa wale nyani, na kwa tabia ya nyani huwa wanapenda sana ndizi, kwa hiyo, yule nyani alimwacha mtoto akakimbilia ndizi ndipo wananchi walipoteremka chini ya bonde na kwenda kumwokoa mtoto. Inasikitisha sana...
Kupitia Bunge lako, naomba Wizara ichukue hatua za haraka sana kuhakikisha inakomesha jambo hili. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kumaliza hilo nitaongelea tena Rombo kwenye upande wa barabara. Alikuja Makamu wa Rais wakati anafungua Hospitali ya Wilaya ya Rombo, akatoa ahadi kwamba atatengeneza barabara inayo...
Tunatambua wazi kwamba, Ziwa Jipe lina magugumaji mengi na yakitolewa, wananchi wa Mwanga watafaidika na samaki na watakuza uchumi wao. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wengi wanakwenda kufanya ziara pale na kila kiongozi anapofika anakutana na malalamiko ya wananchi katika mikutano. Mheshimiwa Mwenyekiti, hata...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nitachangia, ni kuhusu... MWENYEKITI: Mheshimiwa, hitimisha muda wako umekwisha tafadhali. MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri. Sasa namwita Mheshimiwa Minza Simon Mjik...
Namshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Mhagama kwa kazi nzuri ambayo anaifanya, tunaona anavyopambana akiwa jimboni, anaitumikia Serikali yake na anafanya kazi nzuri pamoja na Mawaziri wake. Hongereni kwa kazi nzuri na Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa afya njema ili kazi iweze kwenda vizuri. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti...
Hata tunapokuwa na vikao mbalimbali walimu wanasema hayo yote. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, niende haraka. Napenda niongelee habari ya kikokotoo. Kwa kweli, kikokotoo kinawasumbua sana wafanyakazi na malalamiko haya yamekuwa ni ya muda mrefu. Binafsi niliomba mkae na vyama vya wafanyakazi ili kuweza kukiondoa hiki k...
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna habari ya mapunjo ya mafao ya wastaafu, wengi hawajalipwa, wengi wanalalamika. Ukizunguka katika halmashauri nyingi utaona jinsi ambavyo wastaafu wanavyolalamika, ni wengi. Kila leo napigiwa simu, natumiwa message, jamani tunaomba wale watu basi wapewe mafao yao na walipwe haki zao kwa s...
Wanapofuga kisasa ina maana anakuwa siyo mchungaji, bali ni mfugaji na yule mfugaji mifugo yake ile michache inampatia faida kubwa, kwa sababu atapata maziwa, atauza, atafanya hiki na hiki, maziwa yanamsaidia. Kwa hiyo, anapokuwa na ng’ombe wachache anaweza kuwamiliki vizuri. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nakuja...
Wanatutosha sana kwa ajili ya watalii kuangalia hao tembo, kuliko kuwa wanaua tu watu. Wameua akina mama, akina baba na watoto wanaoenda shule. Kwani tembo anataka kuwa kama nani? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiangalia katika Kitabu cha Maandiko Matakatifu, Hosea 4:6 anasema, “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maa...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepoteza watu wengi. Kweli watu wanapoongea hapa na wengine wanalia wanatoa machozi, ni kweli! Tunapoenda kule kwenye mikutano mbalimbali, mikutano ya ndani na mikutano ya nje swali ni lile lile. Utaongea mambo yote mazuri anayoyafanya Rais wetu, lakini mwisho wa siku akina mama watany...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hili Rais wetu anafanya mambo mazuri sana na inawezekana mambo haya makubwa hayajui jinsi watu wanavyoumia kule tulipo. Tunaomba Serikali yetu isimamie jambo hili ili likome, watu waweze kuishi kwa amani. Hotuba ya Waziri Mkuu ilisema, tunatakiwa kukaa katika hali yenye ulinzi na usa...
PROF. SHUKRANI E. MANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu. Mchana wa leo nitapenda kuchangia katika sehemu iliyopo katika aya ya 215 hadi 218 juu ya Serikali kuhamia Dodoma iliyopo katika ukurasa wa 104 na 105 wa Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu. (Makof...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika kutambua jitihada za Serikali, nitambue kwamba Serikali imeendelea kutekeleza azimio hili la kuhamia Dodoma kwa ufanisi wa hali ya juu. Kwanza ni kwa jinsi ambavyo Serikali imejenga Ikulu, na tutambue kwamba Ikulu hii imesanifiwa na Watanzania wenyewe, Ikulu iliyo katika eneo...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, pia utatambua kwamba mihimili yote kwa kutambua kwamba Serikali imehamia hapa, Bunge linapanua maeneo yake ili kuweza kuweka miundombinu bora kwa ajili ya Wabunge na Watumishi. Pia, mhimili wa Mahakama umejenga jengo kubwa ambalo linaelekea kukamilika la Makao Makuu ya Mahakama hapa Dodo...
Tunapopanga miji yetu, kuna jambo moja linasahauliwa, lilisahauliwa tukiwa bado tupo Dar es Salaam na bado linaendelea kusahauliwa. Hivyo, napenda kuikumbusha Serikali yangu kwamba hili jambo lisiendelee kusahauliwa. Jambo hili ukiangalia katika mipango yake hautaona mahali ambapo Serikali imetenga eneo kubwa zuri la k...
MWENYEKITI: Taarifa, Mheshimiwa Waziri, Jenista Mhagama. TAARIFA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Profesa kwa msisitizo wake wa kuhakikisha tunakuwa na masterplan nzuri kwa ajili ya Jiji la Dodoma, hasa eneo hili la...
Sasa napendekeza mambo yafuatayo: Kama hilo liko katika mpango wa Serikali, unajua unapojenga museum na kama huo ndiyo mpango wetu, sasa mambo haya lazima tuyazingatie. Kwenye museum kimsingi unajua Serikali lazima ijidai, Serikali lazima iji-pride kwamba hii ni mimi na mimi ni Tanzania. Sasa tuna utajiri mkubwa sana, ...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tuwapeleke wageni wetu mahali ambapo tunaweza tukawaonesha kwamba sisi ni Tanzania. Kwa hiyo, sisi tunasema tuna utajiri mkubwa wa madini, lakini utagundua hata hapa ndani, Mheshimiwa Jenista kwa kuwa yeye anatokea Songea atakuwa anajua makaa ya mawe yanafananaje, lakini...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, naona unaangalia muda wako, nimalizie tu kwa kusema kwamba, faida za kuwa na museum itakayokuwa imepangwa vizuri, kKimsingi inatambulisha urithi wetu wa kitamaduni, utajiri wa nchi, na kutunza vema historia ya Tanzania. Katika hilo ninakumbusha tusisahau maktaba nzuri ambayo nayo inaende...
Tunamwomba Mwenyezi Mungu aendelee kuwalinda wenzetu ambao wako katika Ramadhani na tuombe pia atujalie Eid tuisherehekee vizuri. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii pia kukupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wetu na kwa kweli tunakuamini sana. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza san...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuna tatizo moja, katika bajeti ya TAMISEMI mwaka 2023/2024 tulisikia kuna upungufu wa walimu kwa asilimia 51 katika shule za msingi na asilimia 51 katika shule za sekondari. Ukija kwenye takwimu mbalimbali za mwaka huu, utaona tuna upungufu wa walimu pia kwa asilimia 48 kwa ujumla ...
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ukisikiliza michango mingi ya Waheshimiwa Wabunge tangu wakati ule wamependekeza walimu waongezwe na maswali mengi hapa Bungeni huwa yanaonesha kabisa kwamba walimu wanahitajika katika shule zetu. Kwa hiyo, naiomba Serikali izingatie ushauri wa Waheshimiwa Wabunge ili tuweze kutoka hapa tuli...
Kuna upungufu mkubwa wa wataalam wa afya katika hospitali hii. Tunahitaji wataalam zaidi ya asilimia 50, ndiyo upungufu uko hapa. Ukiangalia mfano wa department ya radiology wanatakiwa wawe minimum ya watumishi saba, lakini wapo watatu tu na tuna vifaa pale vingi. Kwa hiyo, vingine vinashindwa kutumika kwa muda unaosta...
Kwa hiyo, nikumbushe Serikali iweze kujenga jengo la mama na mtoto ili tuondokane na hii adha ya kutoa watoto njiti pale Hospitali ya Rufaa Kanda kupeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa Bima ya Afya unategemea sana huduma. Tukiwa na huduma karibu na wananchi, wengi wat...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Ahsante sana, Mungu awabariki. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Anastazia James Wambura kwa mchango wako mzuri. Sasa namwita Mheshimiwa Dkt. Alice Karungi Kaijage atafuatia Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege na Mhes...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Wizara ina mambo mengi sana kwa sababu inaratibu mambo mengi. Nikiwa bado sijajadili sana, kwanza nampongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwasimamia vizuri Mawaziri wetu akiwepo Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Dada yangu Jenista Mhagama Waziri senior, pamo...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vipaumbele vya ule Mpango wa Miaka Mitano kipaumbele namba tano kinahusu ukuzaji wa ujuzi. Kwa hiyo, ina maana ni watu au rasilimali watu. Pia Wizara ya Mipango inajipambanua kwamba, katika kutekeleza mpango huu wa tatu wa Taifa wa maendeleo itazingatia misingi kumi ambayo itawaon...
Ina maana, kuna uhitaji wa watumishi lakini siyo hivyo tu, imefungua kwenye hizo Halmashauri vitengo vya mazingira ya biashara, hivyo, kunahitajika watumishi huko. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napongeza kwamba Serikali imekuja na mfumo mpya wa tathmini na ufuatiliaji, jambo ambalo Wabunge tumepigia kelele sana. ...
Kwanza wanasema amejali maslahi yao; pili, ameboresha mazingira yao ya kufanyia kazi. Kwa hiyo, watu wanaanza na pongezi kwa Mheshimiwa Rais, halafu baadaye ndio wanakuja na changamoto wanazokutana nazo. Kwa hiyo, hii inaonesha kwamba wametambua mchango wa Mheshimiwa Rais ambao tunawapongeza Wizara ya Ofisi ya Waziri M...
Kuna baadhi ya Halmashauri unakuta mtumishi, labda ni Mtendaji Kata amefanya kazi kwa miezi saba, anakwenda na kurudi lakini hajawahi kulipwa posho yake. Wapo wengi wa namna hiyo ambao masilahi yao wanategemea mapato ya Halmashauri. Kuna Halmashauri hazina uwezo, tunakubali, alikuwa anasema Mchangiaji wa Kilolo kwamba ...
Katika Awamu hii ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya miaka mitatu almost, kuanzia Machi, 2021 mpaka Septemba kwa nini watumishi wanamsifu? Ameweza kupandisha vyeo na madaraja zaidi ya watumishi 455,000 ambayo imeigharimu Serikali 1,011,000,000,000/= ndani ya miaka yake mitatu. Siyo hivyo tu, amebadili...
Sasa mtu mzima akisema hivyo, tumpe nafasi, tumwombee kwa Mungu, suala la kikokotoo aweze kufanya maamuzi yaliyo na tija. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Alice Karungi Kaijage. Namwita sasa Mheshimiwa Josephat Sinkamba K...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo anawatumikia Watanzania. Hakika sisi sote na majirani wanajua jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais amejitoa katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Naomba niungane na wenzangu wote ambao wamempongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja n...
Sote ni mashuhuda jinsi ambavyo yamefanyika maboresho makubwa sana katika utoaji wa elimu baada ya hamasa ya elimu bila ada, jinsi ambavyo bajeti imekuwa ikiongezeka ya elimu ya kati na elimu ya juu na hivi karibuni sote tunakumbuka jinsi ambavyo vijana wetu waliongezewa posho ambayo ni maarufu kwa jina la boom kufika ...
Kwanza ni vizuri Serikali wakafuatilia, kwani yapo malalamiko mtaani ambayo yanatokea na hasa upande wa walimu wanaoajiriwa. Tunapata malalamiko kwa vijana pale ambapo yule ambaye alihitimu mwaka 2015 hajaajiriwa lakini mwenzake ambaye wako kwenye kada hiyo hiyo arts amemaliza 2020 amepata ajira. Wanajiuliza, ni criter...
Fursa hii ni vizuri tukaitumia kwa sababu tunao vijana wetu ambao tungependa waajiriwe, lakini nini ambacho tunatakiwa kufanya ili vijana wetu waajiriwe, ambao wataenda kufanya kazi zenye staha? Isije ikawa ilimradi kufanya kazi. Wewe umekuwa ukisikiliza, kuna kipindi tunapata malalamiko, vijana wetu wanaenda kufanya k...
Pale ambapo kunakuwa na malalamiko, inakuwa ni rahisi wao kujua chombo gani wakifikie ili kuweza kupeleka malalamiko yao. Jambo kama hilo tunaweza tukafanya kama Taifa. Unajua zimetangazwa ajira duniani kwa ajili ya kufundisha Kiswahili. Hebu tuambizane kwa jitihada za makusudi, ni chombo gani ambacho kimefanya uratibu...
Personally, alifika mwaka 2020 katika Wilaya ya Kalambo kwenye ziara yake. Wananchi wa Kalambo hususan eneo la Kasanga, wamenituma nimkumbushe maana muungwana akiahidi huwa ni deni. Aliahidi ujenzi wa Kituo cha Afya katika Tarafa ya Kasanga, Kijiji cha Kasanga na tayari eneo lishatengwa, tunasubiri na ninaamini Serikal...
KANYASU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naomba nitumie fursa hii kutambua kazi kubwa na nzuri ambayo inafanywa na Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake wote. Kama ambavyo wamezungumza wachangiaji wengine, ninaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu ikiongozwa na Waziri Mk...
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mtu aliyeanza akasoma certificate ya Wildlife Management anapofikisha miaka 25 kwa mujibu wa taratibu za watu wa maliasili, haajiriki tena. Huyo mtu ana-opt kwenda kusoma kozi nyingine, lakini kwa sababu kwenye mfumo mle ndani tayari anasomeka aliwahi kuingiza Wildlife, ule mfumo unam-r...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la pili, tunaishukuru Serikali kwamba baada ya hali mbaya ya hewa, barabara nyingi sana ziliharibika. Tumepata pesa ya emergency shilingi milioni 400 katika Jimbo la Geita Mjini kwa barabara ambayo inatuunganisha kati ya Geita na Nyang’hwale, lakini pesa hiyo imeenda kujeng...
Naiomba Serikali ifanye takwimu. Mimi kwa miaka mitatu pekee ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nimejenga shule mpya sita. Shule nne nimepata pesa kutoka Wizarani, lakini kwa miaka mitatu wameleta walimu 12. Sasa shule sita on average shule moja inahitaji walimu 24, umeleta walimu 12. Maana yake ni kwamba wali...
Sasa pengine ni vizuri Serikali ikatafuta takwimu kwanza za zahanati ngapi ambazo ziko tayari na zinataka watumishi wangapi ili halmashauri ziache kuwekeza kwenye zahanati. Tena watuzuie kabisa msijenge nyingine mpaka tukamilishe hizi waweze kutuletea nyingine. Vinginevyo tutakuwa tunatumia pesa halafu zahanati zinakuw...
GGM wanakataa kulipa fidia kwa sababu wanasema hakuna sheria. Serikali kwa miaka 24 imeshindwa kuwalazimisha GGM wawalipe fidia watu wa Nyakabale. Matokeo yake vyanzo vya maji vyote vya Nyakabale vinavujiwa na maji machafu; watu wanakosa maji ya kunywa. Hatuwezi kupeleka huduma pale kwa sababu lile eneo huwezi kulipima...
Mkuu wangu wa Idara ya Ardhi alitembelewa na Kamishna wa Ardhi na Kamishna wa Ardhi alikwenda na vyombo vya habari. Akafika akaonesha kwamba kuna mafaili ya watu zaidi ya 100 ambayo hayajashughulikiwa, wanasubiri hati. Mheshimiwa Waziri wa Ardhi akampongeza kwenye Instagram; “Hongera kwa kufanya kazi yako vizuri.” Kesh...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji) MWENYEKITI: Mheshimiwa ahsante. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika moja. MWENYEKITI: Mheshimiwa Constantine Kanyasu, ahsante. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika moja tu namalizia. Sote tunajua haki ya mtumishi...
Ukweli ni kwamba, changamoto zilikuwa ni nyingi sana, nimelia pamoja na Wabunge wengine ambao wanazalisha kahawa na mikoa inayotoa kahawa. Tumeongea mara nyingi tukilia kilio chetu kuhakikisha bei ya zao la kahawa inapanda. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, bei hiyo ilikuwa ikipata changamoto ya tozo kadha wa kadha, laki...
Mtu mmoja ambaye aliathirika anaitwa Jimmy Bagumila Ninondi. Huyu kijana anatokea Kijiji cha Rwabikagati Kitongoji cha Omukagando. Huyu kilichomkuta sasa wakati wanasema huo msako wa kahawa unapita yeye walishamlenga, aligongwa na defender mara mbili, yaani wakamgonga mara ya kwanza, wakahisi kwamba hajafariki vizuri, ...
Sasa wale wanajeshi ambao wanajifanya wanalinda kahawa waliwasha kijiji chote kwa risasi. Nadhani mnakumbuka niliwahi kueleza kwenye briefing, risasi za moto zaidi ya 100 zikarushwa zikatafuta hao wanakijiji. Kama haitoshi, huyu kijana akapigwa risasi ya koromeo akapelekwa Bugando. Nilienza incidence yake ikiwa ni pamo...
Hawa wanajeshi wakala vyakula vyao, wakanywa pombe zao na wakawapiga kwa sababu ya kile kile kinachoitwa kuvusha kahawa. Nataka nieleze wazi, kuna mwingine anaitwa Charles Amos, Mwenyekiti, Afisa Mtendaji Mstaafu wa Kijiji cha Mulongo naye amepigwa kwa sababu anatoa kahawa eneo moja kwenye shamba lake moja kwenda kweny...
Kwa hiyo, ninachokieleza, it is with facts, nakielewa. Naomba niendelee. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu cha pili ambacho nataka nieleze ukiachana... MWENYEKITI: Samahani Mheshimiwa Anatropia. Mheshimiwa Waziri, tafadhali. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, bado naomba uthibitisho w...
Kama Jeshi la Wananchi linafanya tofauti na hayo ambayo yanatarajiwa kufanywa na Jeshi letu, basi naomba andaa taarifa yako yenye vithibitisho na uilete kwenye Meza ya Spika, na Serikali chukueni hiyo taarifa kama alert ili muweze kufuatialia na ninyi muweze kujiridhisha kwa upande wenu. Mheshimiwa Anatropia, endelea. ...
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naiomba Serikali, na nimewahi kumweleza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye kikao kilichofanyika Kyerwa, nikashauri kuwepo na tume ya kwenda kuchunguza na kuondoa changamoto zilizotokea Kyerwa. Hiyo ndiyo nasisitiza kwamba ni lazima ifanyike. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaenda kufungua msimu...
Mheshimiwa Waziri muda wa mzungumzaji ulikuwa umekwisha. Mheshimiwa Anatropia utaandaa taarifa yako yenye vithibitisho na utawasilisha kwenye meza ya Mheshimiwa Spika. Namkaribisha sasa Mheshimiwa Dkt. Florence Samizi, atafuatiwa na Mheshimiwa Benaya Liuka Kapinga na baada ya hapo tutamkaribisha Mohammed Issa, na kama ...
Nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu kwa kazi nzuri anayoifanya, tumemwona anavyokimbia kuhakikisha wananchi wetu wanapata umeme. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama na Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, Naibu Mawaziri na Watendaji wote wa Wizara hii kwa hotuba nzuri waliyotulet...
Wananchi wanapita kwa kulipa pesa, ambapo mtu mmoja shilingi 1,000/= na pikipiki shilingi 3,000/= huku magari hayapiti kabisa. Hii ni Kata ya Rugongwe ambayo katika Jimbo la Muhambwe ndiyo kata inayoongoza kwa uzalishaji wa vyakula. Kwa hiyo, unaweza ukaona ni madhara gani wakulima katika Kata hii ya Rugongwe wanayapat...
Nikisema makorongo, unaweza ukafikiri ni jambo dogo, lakini makorongo ambayo yalikuwa ni mfereji mdogo, sasa yamepanuka sana kiasi kwamba yanaleta madhara makubwa. Makorongo haya yamefikia kiasi yanang’oa miti na hata nyumba. Lile korongo la Migombani pale limeng’oa nyumba ya mwalimu, nyumba ya vyumba vinne imeng’oka k...
Nimeyataja kwa uchache hayo yaliyoko Kibondo Mjini lakini hata Kata za Bitale na Kagezi zina makorongo. Kwa hiyo, madhara ya makorongo katika jimbo hili nayo yanaleta madhara makubwa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, nyumba zinaondoka kwa sababu ya yale maji mengi yanayopita kwenye makorongo, miti inan...
Kupitia wadau tulipambana tukampata mdau wa maendeleo Ernesto akatusaidia kujenga korongo moja ambalo lilikuwa karibu na club ya akina mama kwa teknolojia ya gabion. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, hii teknolojia wanaweka mawe na nyaya na wanapanda miti mle. Hata hivyo, ametengeneza daraja moja tu kwa hii teknolojia ya...
Kwa sababu takwimu zinaonesha kuwa hekta 400,000 za miti zinaendelea kuteketea kila mwaka kwa sababu ya moto kichaa na kukata miti ovyo, pamoja na ukataji miti ambao unatumia vibali maalum, nadhani ni muda muafaka, turejee nyuma tuone zile sheria zilizopitishwa za kuvuna miti, kwamba je, ni kweli tunavuna na kupanda? J...
Kutokulipwa fidia kwa wale wananchi kumesababisha mkandarasi ambaye tayari alikuwa site ashindwe kuendelea na kazi. Wananchi wanadai shilingi bilioni 1.2. Kwa heshima na unyenyekevu naiomba Serikali sikivu iwalipe wananchi hawa ambao wameathirika na barabara hii ili kazi iendelee. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nakush...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza mchango wangu kwa kuijadili hotuba ya Waziri Mkuu kwenye eneo hili la kilimo. Sisi Mbinga Vijijini kama tunavyoitwa vijijini, ni wakulima. Tunalima vizuri kahawa, mahindi, maharage, ngano na mazao mengine. Katika kipindi hiki tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa sababu mvua imenye...
Kwenye zao hili la mahindi hapa karibuni pameibuka hofu kubwa sana kwa sababu mpaka leo ninavyoongea, bado wananchi wana mazao ya mahindi ya mwaka uliopita. Naongelea nini hapa? Kuna shida kubwa ya soko la mahindi ndani ya nchi yetu. Mheshimiwa Mwenyekiti, mahindi ya mwaka 2023 bado hayajaisha na sasa tunakaribia mavun...
Kwa hiyo, naiomba sana Wizara ya Kilimo, imefanya vizuri sana kwenye mambo haya ya input, sasa ifanye vizuri ili baada ya mazao haya tupate masoko. Ipo hofu kwa wakulima hawa kwamba tumefunga mipaka, lakini nina uhakika mipaka haijafungwa. Kwa hiyo, naomba Wizara hii ipite, iwahakikishie wakulima kwamba awamu hii mazao...
(Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeelewa kwamba sasa hivi Serikali inaboresha miundombinu kwenye maeneo haya, kwa hiyo, haipendi sana kuelekea kwenye kugawa, lakini sasa tutoe kipaumbele. Tupeleke hizi huduma kwa namna ya ukubwa wa yale maeneo, ikibidi hata mishahara mimi mwenye Jimbo kubwa, basi nipate mshahara mkubw...
MWENYEKITI: Mheshimiwa Benaya naomba tafadhali hitimisha hoja yako. MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, nitaizungumza wakati mwingine. Naunga mkono hoja. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Benaya. Kwa maslahi ya muda, tutakuwa na mchangiaji mmoja tu ambaye ni Mheshimiwa Mohammed I...
Kadhia iliyowakuta wananchi wa Jimbo la Konde ni kukamatwa, kupigwa na kuzuiwa kufanya shughuli zao za kijamii ikiwemo kuvua na kulima. Namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Hemed Abdalla Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa jinsi walivyolishughulikia suala...
Kwa hiyo, hapa tunataka kujua kwamba je, ni BoT wanaofanya udalali huu au ni benki? Kwa sasabu biashara zinaendelea kama kawaida, lakini fedha za kigeni hazipatikani. Tunataka Serikali ituambie, je, fedha hizi za kigeni zinapatikana kwa njia gani? Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Zanzibar sasa hivi biashara imedumaa, ...