text
string
Majukumu yao katika utoaji wa elimu tajwa ni kama haya yafuatayo: Kushirikiana na wazazi/walezi, walimu na Kamati ya Shule katika kutoa huduma stahiki kwa watoto wa Elimu ya Awali; Kushirikiana na uongozi wa shule katika kuboresha utoaji wa Elimu ya Awali; Kusimamia masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto wa Elimu ya Awa...
Kamati ya MMMAM kwa kila Ngazi ya Utoaji wa Elimu ya Awali Katika utoaji wa Elimu ya Awali, kamati ya MMMAM inayojumuisha wajumbe wote kutoka idara na vitengo vinavyohusika na masuala ya mtoto, itakuwa na majukumu yafuatayo: Kuratibu upatikanaji wa huduma za MMMAM katika ngazi husika; Kutumia matokeo ya tafiti, ufuatil...
Katika utoaji wa Elimu ya Awali, asasi zisizo za kiserikali zina majukumu yafuatayo: Kusaidia juhudi za Serikali katika utoaji wa Elimu ya Awali; Kushirikiana na wadau wengine katika maendeleo ya Elimu ya Awali; Kuchangia rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya Elimu ya Awali; Kushirikiana na Serikali kufanya ufuatiliaji ...
Navyo vimegawanyika katika vipengele vikuu sita ambavyo ni: upatikanaji wa Elimu ya Awali kwa usawa na ujumuishaji; ubora wa elimu itolewayo; utawala bora na uwajibikaji; uwekezaji endelevu katika Elimu ya Awali, uchopekaji wa masuala mtambuko na ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa. Viwango hivi na viashiria vya...
Viwango hivi na viashiria vyake vimewasilishwa kwa njia ya majedwali katika sehemu zinazofuata: Viwango vya Msingi Katika Utoaji wa Elimu ya Awali Viwango vya utendaji katika utoaji wa Elimu ya Awali vimeelezewa kwa kutumia namba 1 hadi namba 4, ambapo namba1(Nyekundu) ikiwa na maana hajaweza, namba 2 (Kijivu) wastani,...
Kipengele Vigezo Viashiria Viwanja vya michezo na vifaa vyake Viwanja na vifaa stahiki vya michezo vinavyokidhi mahitaji ya watoto wote; Michezo rekebifu kwa watoto wenye mahitaji maalumu; Nafasi ya wazi kwa ajili ya viwanja vya michezo mbalimbali; na Vifaa vya michezo ya ndani na michezo ya nje kulingana na mahitaji y...
Kipengele Vigezo Viashiria Samani bora na za kutosha kwa ufundishaji na ujifunzaji wenye ufanisi Madawati, viti na meza kulingana na umri wa mtoto (angalau dawati moja kwa watoto 3); Mikeka, mazulia au turubai kulingana na mazingira; Kabati na shubaka kwa ajili ya kuhifadhi machapisho na vifaa vingine (angalau moja kwa...
Kipengele Vigezo Viashiria Mazingira ya shule Mazingira salama na yenye kuvutia Vyumba vya madarasa vyenye dari kupunguza mwingiliano wa sauti kutoka madarasa jirani; Vyumba vyenye sakafu na madirisha kuzuia vumbi, upepo na mvua pamoja na kuwekewa vizuia radi; Madarasa yenye viti na meza kwa ajili ya watoto pamoja na k...
Kipengele Vigezo Viashiria Mazingira ya shule Mazingira salama na yenye kuvutia Vyumba vya madarasa vyenye dari kupunguza mwingiliano wa sauti kutoka madarasa jirani; Vyumba vyenye sakafu na madirisha kuzuia vumbi, upepo na mvua pamoja na kuwekewa vizuia radi; Madarasa yenye viti na meza kwa ajili ya watoto pamoja na k...
Uzio kuzunguka shule; Stoo ya kutunzia vitu isiyo na unyevunyevu, iwe safi na mwanga wa kutosha; Bendi ya shule; Vifaa vya nje ya darasani ambavyo watoto wanaweza kuvifikia kwa urahisi na kuvitumia; Kipengele Vigezo Viashiria . Alama za tahadhari katika mazingira hatarishi. Suhura za michezo zenye vifaa salama kwa wato...
Suhura za michezo zenye vifaa salama kwa watoto; Vifaa vya kuzimia moto zikiwamo ndoo na mchanga; Vitabu vya kutunzia kumbukumbu na vinavyoonesha taarifa za ukarabati; Bwalo liwe mbali na jiko, lifanyiwe usafi, liwe na mwanga, viti na meza au mikeka kwa ajili ya watoto wote, wakiwamo wenye ulemavu; Vyumba vya madarasa ...
Uhusiano chanya kati ya mwalimu na mtoto Ushirikiano chanya kati ya mwalimu na mtoto; Ushirikishwaji wa watoto katika michezo ya ndani na nje ya darasa; Huduma za uangalizi kutoka kwa msaidizi wa mwalimu; Mbinu rekebishi ambazo ni rafiki za kudumisha nidhamu ya mtoto zinazoendana na umri wake; Kipengele Vigezo Viashiri...
Huduma muhimu kwa watoto Chakula na lishe Huduma ya chakula/uji kwa kuzingatia uwiano wa viinilishe; Jiko bora, vifaa vya jikoni na vyombo vya kulia chakula; Taarifa za afya za walimu, wapishi, wahudumu na wasaidizi wa mwalimu kila baada ya miezi 6; 81 Kipengele Vigezo Viashiria Maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono...
Kipengele Vigezo Viashiria Mazingira stahiki kwa afya ya mtoto Sanduku la huduma ya kwanza pamoja na dawa na vifaa tiba vyake; Maji safi na salama ya kunywa darasani na katika sehemu inayoweza kufikiwa na watoto wote; Takwimu za vipimo vya uzito na urefu wa mtoto kila baada ya miezi mitatu; Sehemu salama ya kuhifadhia ...
Kipengele Vigezo Viashiria Ushiriki wa jamii katika kutoa huduma Ratiba za vikao vya wazazi; Kumbukumbu za vikao kulingana na ratiba; Kiongozi cha mafunzo kwa walimu na jamii katika kutoa huduma stahiki kwa mtoto; Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule unaobainisha vipaumbele; Taarifa za ushirikishwaji wa jamii katika z...
Vigezo Kipengele Kipengele Vigezo Viashiria Miundombinu Majengo muhimu, stahiki na ya kutosha kwa kuzingatia mahitaji ya watoto Vyumba imara vya madarasa vyenye: Madirisha yanayoruhusu mwanga na hewa ya kutosha; Madirisha pande mbili ambayo yanafunguka kwa kupishana ambayo ukubwa wake ni asilimia 20 ya eneo la sakafu y...
Ukubwa wa darasa lenye vipimo vya mita 6 kwa mita 8 nafasi ya ndani yenye uwezo wa kubeba watoto 25 (Mita za eneo 1.9 kwa kila mtoto). Kipengele Vigezo Viashiria Kona zenye mpangilio wa zana/ vifaa kulingana na muktadha wa ujifunzaji; Madawati, viti na meza kulingana na mahitaji na umri wa watoto; Vyumba vya madarasa k...
Kipengele Vigezo Viashiria Kona zenye mpangilio wa zana/ vifaa kulingana na muktadha wa ujifunzaji; Madawati, viti na meza kulingana na mahitaji na umri wa watoto; Vyumba vya madarasa kulingana na idadi ya watoto; Darasa linaloongea lenye zana zilizotundikwa na kubandikwa ukutani kulingana na muktadha wa ujifunzaji; Ki...
Mtaala Mtaala ulioandaliwa na mamlaka yenye dhamana ya ukuzaji mitaala Mtaala wa Elimu ya Awali ulioidhinishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania; Vitabu na machapisho yaliyoidhinishwa; Vifaa vya mtaala vilivyopata ithibati; 92 Viashiria Taarifa ya kuchambua mtaala, muhtasari vitabu vya kiada na machapisho mengine; Taarifa z...
Vigezo Kipengele Kipengele Vigezo Viashiria Mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji Ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia ukuzaji wa umahiri, ujenzi wa maana kwa kutumia mazingira wezeshi yanayokidhi mahitaji na uzoefu/ utamaduni wa mtoto Taarifa mbalimbali za ushiriki wa watoto katika shughuli mbalimbali za ujifunzaji;...
Maandalizi ya ujifunzaji na ufundishaji Maazimio ya kazi; Andalio la somo kwa kila kipindi cha ujifunzaji; Shajara kwa kurejea umahiri; na Vitabu na machapisho mengine. Kipengele Vigezo Viashiria Stadi za awali za Kusoma, Kuandika, Kuhesabu (rejea Kiongozo cha utekekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Uendeshaji na Viwan...
Kipengele Vigezo Viashiria Stadi za awali za Kusoma, Kuandika, Kuhesabu (rejea Kiongozo cha utekekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Uendeshaji na Viwango katika Elimu ya Awali) Ujifunzaji wa mtoto Vitendo vya mtoto darasani na nje ya darasa kurejea katika mtiririko wa muhtasari na andalio katika umahiri: Kuthamini utam...
Kipengele Vigezo Viashiria Vifaa/Zana za kufundishia na kujifunzia Zana stahiki kwa uwiano kulingana na mahitaji ya mtoto; Vitabu vya kiada kwa uwiano wa 1:1; Vitabu vya ziada kwa uwiano wa 1:2; Vifaa vya watoto wenye ulemavu kwa uwiano wa 1:1 kwa kila kifaa; Vibao vya kujifunzia kwa uwiano wa 1:1; Kipengele Vigezo Via...
Kipengele Vigezo Viashiria Maendeleo ya mtoto Ufuatiliaji wa maendeleo ya mtoto kwa kila umahiri Taarifa za sensa iliyoongozwa na Afisa Elimu Kata na kumshirikisha mwalimu wa Elimu ya Awali; Taarifa za upimaji chekeche; Ubora wa kazi za mtoto kwa kurejea umahiri (upimaji wa matokeo ya ujifunzaji katika vipindi tofauti ...
Upimaji wa matokeo ya ujifunzaji Zana za upimaji wa matokeo ya ujifunzaji; Michezo inayotumika kama vichocheo (stimuli) vya upimaji badala ya mitihani; Kipengele Vigezo Viashiria Mwongozo unaobainisha zana na viashiria vilivyopendekezwa vya upimaji wa matokeo ya ujifunzaji; Ratiba za upimaji wa matokeo ya ujifunzaji; T...
Kipengele Vigezo Viashiria Mafunzo endelevu kazini kwa walimu Mpango wa utoaji wa mafunzo endelevu ya walimu kitaalamu ikiwamo elimu jumuishi (kupitia vituo vya walimu - TRCs au jumuiya za ujifunzaji shuleni); Mpango wa mafunzo endelevu kwa walimu wa kuwawezesha kujenga uwezo wa kitaaluma na kitaalamu; Taarifa za walim...
Mwalimu wa Elimu ya Awali Sifa na umahiri wa mwalimu wa Elimu ya Awali Walimu waliohitimu mafunzo ya ualimu Elimu ya Awali kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali; Taarifa za ujifunzaji wa mtoto wa Elimu ya Awali kulingana na mahitaji na umri wake; Taarifa za uchunguzi darasani zinazobainisha matumizi ya mbinu shiriki...
Taarifa za ushiriki katika jumuiya za ujifunzaji; Taarifa za matumizi ya rasilimali kwa ufanisi; na 12. Uchopekaji wa masuala mtambuko katika uwezeshaji wa ujifunzaji wa watoto. Fursa ya walimu kujiendeleza kitaalamu na kitaaluma Taarifa za walimu waliopata fursa za kujiendeleza kitaalamu na kitaaluma, ikiwamo ya Elimu...
Kumbukumbu zinazoonesha matumizi ya TEHAMA; Orodha ya walimu wenye ujuzi wa TEHAMA; Taarifa za ujifunzaji wa watoto kwa kutumia TEHAMA; na Taarifa za utoaji wa mafunzo ya TEHAMA. Uthibiti Ubora wa Shule Ushauri wa kitaalamu kuhusu Elimu ya Awali Taarifa za ziara za uthibiti ubora wa shule kuhusu Elimu ya Awali; Mahitaj...
Kipengele Vigezo Viashiria Uthibiti Ubora wa Ndani ya Shule (Mkuu wa Shule, Timu ya Uthibiti Ubora wa Shule na Kamati ya Shule) Taarifa za usimamizi mahsusi kwa ajili ya ushiriki wa mwalimu mkuu katika uboreshaji wa ujifunzaji na ufundishaji katika Elimu ya Awali; Taarifa za shule kujitathmini yenyewe; na Taarifa za ur...
Uthibiti Ubora wa shule (AEK) Taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya Elimu ya Awali; Taarifa za vikao vya kupeana mrejesho wa maendeleo ya Elimu ya Awali; Mpango wa utaratibu wa jumuiya za ujifunzaji kwa walimu wa Elimu ya Awali; Ratiba ya kutembelea shule, zikiwamo za Elimu ya Awali zilizopo katika kata; n...
Vigezo Kipengele Kipengele Vigezo Viashiria Uongozi na Utawala wa Shule Uongozi unaohusisha watendaji mbalimbali wa Elimu Kamati ya Shule iliyo hai; Kumbukumbu za vikao vya kawaida vya walimu vilivyojadili masuala ya Elimu ya Awali angalau kila mwezi; Kumbukumbu za vikao vya walimu na wazazi/walezi angalau mara mbili k...
Uwazi katika kuongoza shule Mabango ya matangazo yenye taarifa muhimu, zikiwamo taarifa za mapato na matumizi ya shule/darasa la Elimu ya Awali; Sanduku la maoni la kukusanyia taarifa za uendeshaji wa shule kutoka kwa wadau wote, wakiwamo watoto wa Elimu ya Awali; Kipengele Vigezo Viashiria Taarifa za utekelezaji wa ma...
Uimarishaji wa usimamizi wa shule Majukumu ya wadau katika kuimarisha usimamizi wa shule ya Awali au darasa la Elimu ya Awali; Walimu waliopatiwa mafunzo ya Elimu ya Awali; Kamati za Shule zilizopata mafunzo katika kusimamia maendeleo ya shule ya Elimu ya Awali; Viashiria Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule unaojumui...
Vitabu vya fedha na risiti za malipo; Taarifa za ukaguzi wa fedha na kuhuisha mali za shule; na 12. Taarifa za hesabu za fedha za shule. Walimu na watumishi mwega Walimu wenye shahada I & II, stashahada na cheti; Walimu wasaidizi wenye shahada, stashahada na cheti; Kipengele Vigezo Viashiria Wasaidizi wa walimu wa kuji...
Rasilimali Muda Matumizi stahiki ya muda katika Elimu ya Awali Ratiba za utekelezaji; Kalenda ya utekelezaji; Mpango kazi; Mrejesho wa kazi; na Ajenda za utekelezaji. Kipengele Vigezo Viashiria Magonjwa Utoaji wa elimu ya magonjwa yanayoathiri ukuaji wa watoto Programu ya mafunzo ya familia bora, VVU na UKIMWI, Afya ya...
Kipengele Vigezo Viashiria Magonjwa Utoaji wa elimu ya magonjwa yanayoathiri ukuaji wa watoto Programu ya mafunzo ya familia bora, VVU na UKIMWI, Afya ya akili na mwili Programu ya mafunzo ya magonjwa ya mlipuko; Programu ya mafunzo ya magonjwa mengineyo ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa; Huduma za uangalizi na u...
Kipengele Vigezo Viashiria Huduma ya Uangalizi na Usaidizi Utoaji wa huduma ya msaada wa Kisaikolojia na kijamii kwa ufanisi kwa watoto wa Elimu ya Awali Wanasihi wenye sifa shuleni angalau wawili (mwanamume na mwanamke); Chumba cha unasihi shuleni; Programu za ushauri na unasihi; Ratiba za ushauri na unasihi; Kumbukum...
Programu za utoaji wa chakula kwa ufanisi katika Elimu ya Awali Ratiba ya utoaji wa mlo kamili (wenye virutubisho vyote) angalau mara moja kwa siku; Orodha ya mlo kamili; Leja ya mapato na matumizi; Kipengele Vigezo Viashiria Leja ya vifaa vya chakula; Stoo ya utunzaji wa chakula; Kumbukumbu za kamati ya shule kujadili...
Kipengele Vigezo Viashiria Huduma za afya kwa watoto wa Elimu ya Awali Mwalimu mtaalamu wa afya; Sanduku la Huduma ya Kwanza lenye dawa muhimu na vifaa tiba muhimu; Uratibu wa utoaji rufaa kwa watoto wenye kuhitaji uangalizi wa karibu zaidi na utunzaji wa kumbukumbu; Utaratibu wa kukagua afya za watoto kila mara (ikiwa...
Kipengele Vigezo Jinsia Jumuiya ya shule kuwa na uelewa wa mambo ya jinsia kwa watoto wa Elimu ya Awali Zana za kujifunzia, taarifa na elimu zinazozingatia jinsia; Taarifa za tafiti zilizofanywa kuhusu kuwapo kwa vikwazo vinavyoathiri ushiriki sawia katika ujifunzaji; Mpango wa kutoa mafunzo kwa walimu na wanajumuiya y...
Dharura na utayari wa kukabili majanga Ufanisi katika kukabili majanga kwa watoto wa Elimu ya Awali Mifereji ya maji inayoondoa maji ya mvua shuleni; Vidhibiti radi katika majengo ya shule; Vifaa vya kuzima moto; Viashiria Milango ya dharura inayofunguka kwa nje; Mpango wa utoaji wa elimu ya ulinzi na usalama, ikiwamo ...
Vigezo Kipengele Kipengele Vigezo Viashiria Ufuatiliaji na tathmini Mchakato wa ufuatiliaji na tathmini katika utoaji wa Elimu ya Awali kwa ufanisi Utaratibu wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa ya Elimu ya Awali; Taarifa za wadau wa Elimu ya Awali walioshirikishwa; Hadidu za rejea na madodoso ya ufuatiliaji n...
Kipengele Vigezo Viashiria Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu (MTUE) Utumiaji wa mfumo wa taarifa za usimamizi wa elimu katika shule Kanzidata inayohusisha taarifa za Elimu ya Awali; Taarifa za matukio ya kila siku ndani na nje ya shule; Taarifa za shughuli na viwango vya utendaji wa shule zilizotolewa kwa wadau ku...
Kipengele Vigezo Viashiria Utafiti wa kielimu Matumizi sahihi ya utafiti katika kutatua matatizo ya kielimu katika ngazi ya shule au jamii kuhusu Elimu ya Awali Taarifa za tafiti katika masuala ya ujifunzaji na ufundishaji; Kumbukumbu za ushiriki wa wazazi/walezi na jamii katika zoezi la sensa ya kufanya utambuzi wa aw...
SEHEMU YA NNE UFUATILIAJI NA TATHMINI YA ELIMU YA AWALI Utangulizi Sehemu hii inaeleza namna utekelezaji wa Mwongozo wa Uendeshaji na Viwango katika Elimu ya Awali (MUVEA) utakavyopimwa. Upimaji huu unaitwa upimaji na tathmini. Ufuatiliaji na tathmini utafanyika kwa kuzingatia viashiria vilivyotolewa katika jedwali la ...
Ufuatiliaji na Tathmini kwa Kuzingatia Viashiria Ufuatiliaji na tathmini kwa kila ngazi utafanyika kwa kupima matokeo ya utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kutekelezwa ili kuona ni kwa kiasi gani zimetekelezwa. Ufuatiliaji utabaini mazuri yaliyofanyika pamoja na dosari zote zilizojitokeza na kutoa mapendekezo ya kubo...
Viashiria vya msingi vitakavyotumika kupima utekelezaji wa mwongozo huu vimetokana na malengo mahsusi yaliyobainishwa. Viashiria hivyo vimefafanuliwa katika vipengele vinavyofuata. Viashiria vya Utekelezaji kutokana na Lengo la “Kubainisha Mahitaji Stahiki katika Uendeshaji na Utoaji wa Elimu ya Awali” Maeneo yanayohit...
Viashiria vya Utekelezaji kutokana na Lengo la “Kubainisha Mahitaji Stahiki katika Uendeshaji na Utoaji wa Elimu ya Awali” Maeneo yanayohitajika kupimwa katika lengo hili ni pamoja na: Kuwapo kwa ardhi inayomilikiwa kihalali; Kuwapo kwa miundombinu stahiki; Kuwapo kwa walimu wenye sifa stahiki; Kuwapo kwa wasaidizi wa ...
Viashiria vya Utekelezaji kutokana na Lengo la “Kubainisha Majukumu ya Wadau Mbalimbali katika Uendeshaji na Utoaji wa Elimu ya Awali” Eneo hili litafuatiliwa kuona ni kwa kiwango gani majukumu ya wadau wa elimu yamebainishwa. Aidha, litafuatiliwa ili kuona uzingatiaji wa namna jamii inavyoshirikishwa ili kutimiza waji...
Mambo yatakayozingatiwa ni pamoja na kuangalia: Idadi ya vikao vya wazazi vilivyofanyika kuhamasisha uandikishaji na utoaji wa huduma stahiki kwa watoto wote; Idadi ya vikao vilivyohusisha walimu na kamati ya shule ili kubaini mafanikio na changamoto za ufundishaji na ujifunzaji, na maendeleo ya watoto/ wanafunzi kwa u...
Wahusika katika Ufuatiliaji na Tathmini Wahusika wa zoezi la ufuatiliaji na tathmini katika Elimu ya Awali watakuwa: mwalimu wa darasa, mwalimu mkuu, kamati ya shule, wazazi/walezi, Afisa Elimu Kata na wamiliki wa shule za awali zisizo za serikali. Wadau wengine wa Elimu ya Awali ni Mratibu Elimu ya Awali Wilaya, Mthib...
Majukumu ya Wafuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Awali Kila mhusika atatekeleza majukumu yake kulingana na Mwongozo unavyoelekeza katika ngazi husika. Hata hivyo, majukumu yafuatayo hayana budi kutekelezwa wakati wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Awali: Kufuatilia ...
Hata hivyo, majukumu yafuatayo hayana budi kutekelezwa wakati wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Awali: Kufuatilia mabadiliko ya ukuaji na maendeleo ya ujifunzaji wa mtoto wa Elimu ya Awali; Kuwatambua na kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu wa Elimu ya Awali; Kuhakikisha walimu wa Elim...
Mbinu Zinazotumika katika Kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ya Elimu ya Awali Mbinu mbalimbali zitatumika kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mikakati iliyowekwa katika kutekeleza shughuli za maendeleo ya Elimu ya Awali. Baadhi ya mbinu hizo ni: Kufanya mikutano mbalimbali na wadau; Kuangalia taarifa mbalimbali za utekele...
Hivyo, wanatakiwa kujua ni maeneo gani yanatakiwa kufanyiwa ufuatiliaji na tathmini katika Elimu ya Awali ili kubaini mafanikio na mapungufu katika maeneo hayo. Hii itasaidia kupata suluhisho la upungufu na kusaidia Elimu ya Awali kutolewa kwa ufanisi. Kuna maeneo makuu matatu ambayo wanakamati, mkuu wa shule na wadau ...
Utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Awali Katika utekelezaji wa Mtaala na Muhtasari wa Elimu ya Awali, mwalimu mkuu, kamati ya shule na wadau wengine wanatakiwa kufuatilia na kutathmini mambo yafuatayo: Mahudhurio ya mwalimu wa Elimu ya Awali; Mahudhurio ya watoto/wanafunzi shuleni; Ufanisi wa kazi za walimu wa Elimu ya ...
Rasilimali Zinazotumiwa katika Elimu ya Awali Katika eneo hili, mwalimu mkuu, kamati ya shule, na wadau wengine wanatakiwa kufanya ufuatiliaji na tathmini katika: Masuala ya fedha zilizotumika katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Elimu ya Awali (mapato na matumizi); Muda (taratibu za kila siku za utolewaji wa Eli...
Utawala na Usimamizi Katika eneo hili, wadau wa Elimu ya Awali wana wajibu wa kufanya ufuatiliaji na tathmini katika: Masuala ya mawasiliano; Utunzaji wa nyaraka mbalimbali za Elimu ya Awali; Nidhamu ya mwalimu na watoto/wanafunzi wa Elimu ya Awali; Masuala Mtambuko; Ustawi wa jamii (huduma za afya, nyumba ya mwalimu, ...
Mwongozo wa Kuandaa na Kutumia Vifaa vya Michezo kwa watoto Wadogo. Programu ya Mafunzo Kazini kwa Walezi wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo Mchana na Walimu wa Elimu ya Awali. Dar es salaam: Wizara ya Elimu na Utamaduni. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2013b) Mwongozo wa Utambuzi wa Mapema wa watoto Wenye Mahitaji M...
Pediatrics, 107(6) Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN). (2013). Kiunzi cha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Tanzania. Dar es Salaam: TECDEN. Naudeau, S., Kataoka, N., Valerio, A., Neuman, M. J. & Elder, L. K. (2010). Investing in young children: An early childhood deve...
Mtaala na Muhtasari wa Elimu ya Msingi. Dar es Salaam: TET. Taasisi ya Elimu Tanzania (2016). Mtaala na Muhtasari wa Elimu ya Awali. Dar es Salaam: TET. Taasisi ya Elimu Tanzania (2016). Mwongozo wa Mwalimu wa Kufundishia Elimu ya Awali. Dar es Salaam: TET. Tanzania Teachers’ Union (2020). Competence Profile for Early ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) TAARIFA YA MWAKA YA SHUGHULI ZA KAMATI KWA KIPINDI CHA FEBRUARI 2022 HADI FEBRUARI 2023 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 136 (15) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020) Idara ya Kamati za Bunge S.L.P. 941...
Jicho la Bunge katika kushugulikia maeneo yenye matumizi mabaya ya fedha za umma katika wizara za Serikali na mashirika ya umma ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC). Majukumu ya PAC yameainishwa katika Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Juni, 2020 ambapo msingi wa utekelezaji wa majukumu hayo ni Ta...
Baada ya uchambuzi wa Taarifa za Fedha (financial audit reports), Kamati ilitoa Taarifa yake hapa Bungeni mapema mwezi Novemba, 2022 ambapo ilijadiliwa kikamilifu. Vilevile, Kamati imefanya uchambuzi katika Taarifa za ukaguzi wa kiufundi, ukaguzi wa kina na ukaguzi wa ufanisi. Baadhi ya masuala yaliyobainika kuwa na ch...
Kwa upande wa ukaguzi wa kiufundi, Kamati imefanya uchambuzi wa kina na kuangalia iwapo kuna thamani ya fedha za umma katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Kwa muktadha huo, maeneo yaliyobainika kuwa na mapungufu ni pamoja na dosari za kiusimamizi katika miradi teule ya usambazaji wa maji, mapungufu kat...
Kamati imependekeza kuwa, Serikali ifanye malipo kwa wakandarasi kwa wakati ili kuepusha hasara ambayo Taifa linapata kutokana na ulipaji wa riba. Aidha, kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za umma, Serikali ihakikishe inawasilisha kwa CAG taarifa ya kila robo mwaka ya utekelezaji ...
Mheshimiwa Spika, Msingi wa majukumu hayo unatokana na Taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kama ilivyobainishwa katika Kifungu cha 16 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020. Miongozo Iliyotumika na Namna Kamati Ilivyotekeleza Majukumu ...
Miongozo Iliyotumika na Namna Kamati Ilivyotekeleza Majukumu yake Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ilifanya rejea ya kina katika nyaraka zifuatazo: - Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977; Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (2020/21); Taarifa za kaguzi mahsusi (...
Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ilitumia mbinu zifuatazo: - Kupokea, kuchambua na kujadili maelezo mafupi “briefs” za CAG kuhusu hoja za ukaguzi za mafungu husika; Mahojiano na Maafisa Masuuli kuhusu hoja za ukaguzi; Uchambuzi wa kina wa taarifa za ukaguzi za mafungu mahususi; Ziara za ukaguzi...
Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ilijielekeza katika kubainisha namna taasisi za Serikali zilivyotumia fedha za umma katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali. Mheshimiwa Spika, Kwa kutumia Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na mashirika ya umma kw...
Mheshimiwa Spika, Katika kuwawezesha Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati kutimiza majukumu yao kwa weledi na ufanisi, njia mbalimbali za kuwajengea uwezo zilifanyika ikiwa ni pamoja na semina na mafunzo. Mheshimiwa Spika, Kwa maelezo ya kina, shughuli zilizotekelezwa na Kamati katika kipindi tunachokitolea taarifa ni kama if...
Mheshimiwa Spika, Kwa maelezo ya kina, shughuli zilizotekelezwa na Kamati katika kipindi tunachokitolea taarifa ni kama ifuatavyo: - Uchambuzi wa Taarifa za Hesabu Zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi Nyinginezo kwa Mwaka wa Fedha Unaoishia Tarehe 30 Juni, 2021 Mheshimiwa Spika, Katika kipindi ch...
Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 1431 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, alikamilisha kaguzi na kutoa hati za ukaguzi kwa jumla ya Taasisi 331 za Serikali Kuu ikijumuisha Wizara na Idara zinazojitegemea, W...
Vilevile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alikamilisha Kaguzi za Ufanisi 12 ambapo taarifa hizo ziliwasilishwa mbele ya Kamati na kujadiliwa ipasavyo. Mheshimiwa Spika, Katika ngazi ya Kamati, Kamati ilifanikiwa kuchambua na kujadili taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za mafungu 12 ya serikali kuu, mashirik...
Kifungu hicho kinampa jukumu la moja kwa moja 1 Mamlaka na majukumu ya kisheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (personal liability) Afisa Masuuli husika katika uwajibikaji na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma kwenye fungu husika. Mheshimiwa Spika, Kufuatia uchambuzi wa taarifa husika na mahojian...
Mheshimiwa Spika, Kwa upande mwingine hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2021 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu alikamilisha kaguzi za kiufundi (technical audit), kaguzi za ufanisi (performance audit) na kaguzi za kina (comprehensive audit) kwa jumla ya sekta na miradi tisa (9) ya maendeleo. Napenda kulifahamisha Bunge lako...
Kaguzi hizo ambazo zimepitiwa na kuchambuliwa na Kamati tarehe 16 hadi 27 Januari, 2023 ni kama ifuatavyo: - Taarifa ya Ukaguzi wa Kiufundi Kuhusu Usanifu na Usimamizi wa Miradi Teule ya Usambazaji wa Maji; Taarifa ya Ukaguzi Maalum wa Ujenzi, Ukarabati na Uboreshaji wa Viwanja vya Ndege; Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi ...
Kaguzi hizo ambazo zimepitiwa na kuchambuliwa na Kamati tarehe 16 hadi 27 Januari, 2023 ni kama ifuatavyo: - Taarifa ya Ukaguzi wa Kiufundi Kuhusu Usanifu na Usimamizi wa Miradi Teule ya Usambazaji wa Maji; Taarifa ya Ukaguzi Maalum wa Ujenzi, Ukarabati na Uboreshaji wa Viwanja vya Ndege; Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi ...
Naomba kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa uchambuzi yakinifu wa matokeo ya kaguzi hizo umejumuishwa katika aya 2.3 ya taarifa hii. Matokeo ya Uchambuzi wa Taarifa za Kaguzi za Kiufundi, Kaguzi za Kina na Kaguzi za Ufanisi Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 16 Januari hadi tarehe 27 Januari, 2023, Kamati...
Mheshimiwa Spika, Kwa muhtasari naomba kutoa maelezo mafupi kuhusu aina, malengo na tafsiri ya kaguzi hizi kama ifuatavyo: - Ukaguzi wa Ufanisi (Performance Audit) Ni aina ya ukaguzi uliojikita kuangalia kama kuna Uwekevu, Tija na Ufanisi (economy, efficiency and effectiveness) miongoni mwa taasisi za umma katika matum...
Ukaguzi wa kiufundi ni ukaguzi katika mchakato mzima wa utekelezaji wa mradi kuanzia hatua ya maandalizi ya awali, utekelezaji wa mradi, ukamilishaji na makabidhiano ya mradi. Hujikita zaidi kutazama kama mradi umetekelezwa kwa wakati, ndani ya gharama iliyokusudiwa, kwa ubora uliokusudiwa na kama malengo ya uanzishwaj...
Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo hayo ya ufafanuzi, naomba kusisitiza kuwa Taarifa hizi ni muhimu kwa kuwa zinahusu ukaguzi wa fedha zilizotumiwa na Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika maeneo tisa (9). Kaguzi za aina hii hulenga kuangalia kiwango cha uzingatiaji wa taratibu, sheria na ka...
Aidha, hoja hizo hazikuwa zimefungwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kuwa hazikuwa na majibu ama vielelezo vya kujitosheleza. Mheshimiwa Spika, Matokeo ya uchambuzi wa taarifa hizo kwa kila moja ni kama ifuatavyo: - Uchambuzi wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Mifuko ya Uwezeshaji Wa...
Mheshimiwa Spika, Katika jitihada za kuongeza ushiriki wa Watanzania katika sekta ya fedha, Serikali iliamua kuweka mkazo kwenye kutanua huduma za kifedha hususani kwa watu wenye kipato cha chini. Miongoni mwa mikakati iliyochukuliwa na Serikali ilikuwa ni pamoja na; kuanzisha Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi amb...
Katika ukaguzi huu, CAG aliongozwa na sababu kuu tatu (3) zifuatazo: - Dosari Katika Usimamizi wa Mifuko ya Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi Mapitio ya Taarifa za Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ya mwaka 2019, yalibainisha uwepo wa mifuko takribani 13 kati ya 52 inayomilikiwa na Serikali ambayo inat...
Pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini kuwa kiasi cha Shilingi Milioni 126.9 tu kati ya Shilingi Bilioni 1.159 ya mikopo yote iliyotolewa sawa na asilimia 11 iliweza kurejeshwa; na Mikopo Inayotolewa Kutowafikia Walengwa Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi haijawafikia walengwa na ma...
Ukaguzi ulihusisha mikoa miwili (2) ya Dodoma na Dar es Salaam, hii ni kwa sababu makao makuu ya wakaguliwa yapo kwenye mikoa hii. Ukaguzi ulihusisha kipindi cha miaka minne (4) ya fedha kuanzia mwaka 2017/18 hadi mwaka 2020/21. Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo hayo naomba kulifahamisha Bunge lako Tukufu matokeo ya u...
Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, ulikuwa na mikopo chechefu ya Shilingi Bilioni 20.1 kati ya Shilingi Bilioni 27.87 ya fedha zote zilizokopeshwa, kiwango ambacho ni sawa na asilimia 72; Mfuko wa Kilimo Kwanza ulikuwa na mikopo chechefu ya Shilingi Bilioni 27.6 kati ya Shilingi Bilioni 34.2 ya fedha zote zilizokopeshwa, saw...
Mikopo hii chechefu ilichangiwa zaidi na kutoa mikopo kwa watu wasiokuwa na sifa; Fedha Kutopelekwa Kwa Makundi Yaliyokusudiwa Ukaguzi ulibaini kuwa Mfuko wa Kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF MF) uliwekeza kiasi kikubwa cha fedha sokoni kwenye dhamana na kutoa mikopo kwa benki za biashara ambayo haiendani na ...
Mathalani, kwa kipindi cha mwaka wa fedha kuanzia Juni, 2017/18 hadi 2020/21, kiasi cha mkopo chenye thamani ya Shilingi Bilioni 72.2 (sawa na asilimia 56) toka Mfuko wa Kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF MF) kilitolewa kwa benki za biashara badala ya kutoa mkopo kwa wajasiriamali waliopo kwenye maeneo ambayo ...
Kushindwa kutoa dhamana kwa maombi ya mikopo hiyo kulisababishwa na kumalizika kwa muda wa Mkataba wa Uwakala kati ya Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania tangu tarehe 8 Julai, 2008. Kutokana na hali hii, lengo kuu la mfuko huu la kukuza uchumi kupitia kuuza bidhaa nje ya nchi kwa lengo la kuongeza fursa...
Kutokana na hali hii, lengo kuu la mfuko huu la kukuza uchumi kupitia kuuza bidhaa nje ya nchi kwa lengo la kuongeza fursa za ajira na kuongeza mapato kupitia fedha za kigeni linaweza lisifikiwe; Dhamana za Mikopo Kwenye Mfuko wa Dhamana ya Mikopo ya Kuuza Nje zilizotolewa Kinyume na Miongozo Kifungu Namba 8.1 cha Sera...
Mapitio ya Taarifa ya Utekelezaji ya mwaka 2020, yanaonesha kuwa, kiasi cha Shilingi Bilioni 84 cha dhamana kilitolewa ikiwa ni kiwango cha juu kupita viwango elekezi; Shilingi Bilioni 7 za Mfuko wa Wakulima Wadogo Katika Benki ya Kilimo Kutotumika kwa Malengo Husika Muongozo wa Usimamizi wa Mfuko wa Dhamana wa Wakulim...
Ukaguzi ulibaini kuwa, asilimia 88 (sawa na mifuko 46 kati ya 52) ya mifuko hiyo ilikuwa inatoa mikopo, dhamana, ruzuku, na programu zingine za uchumi. Asilimia 12 (sawa na mifuko 6 kati ya 52) ya mifuko hiyo ilijikita katika urejeshaji wa mikopo na haitoi mikopo mipya. Ukaguzi ulibaini kuwa, uwepo wa mifuko mingi amba...
Ukaguzi ulibaini kuwa, uwepo wa mifuko mingi ambayo inalenga kutoa huduma zilezile umechangiwa na kutoanza kazi kwa Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji kwa miaka 17 sasa toka kuanzishwa kwake kwa mujibu wa Vifungu Namba 16 na 17 vya Sheria ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004; na Dosari Katika Ufuatiliaji wa Mifuko y...
Mheshimiwa Spika, Usimamizi mzuri wa miradi utahakikisha kwamba urejeshaji wa mikopo unaanza pindi ambapo miradi inatoa huduma. Hivyo, ni muhimu kwa Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha kwamba maswala yote yanayoweza kuathiri ukamilishaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa wakati yanapatiwa ufumbuzi. Mheshimiwa Spi...
Mheshimiwa Spika, Jambo kubwa lililochangia kufanyika kwa ukaguzi huu ni uwepo wa kiasi cha Shilingi Trilioni 11.96 kilichopangwa kutumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (5) kuanzia 2016/17-2020/21. Kiasi hicho cha fedha kilipangwa kutumika ili kuweza kufikia m...
Kwa mfano kutokana na changamoto hizi, ilisababisha kuchelewa kulipa fidia kwa waathirika wa mradi kwa siku zaidi ya 300 kwa miradi 2. Kuchelewa huko kulisababisha mradi kuchelewa kuanza na ongezeko la gharama za utekelezaji kwa Serikali. Miradi iliyochelewa kutokana na kuchelewesha fidia ni ule wa Kuwezesha Biashara n...
Aidha, ilibainika kuwa Idara ya Mipango ya Taifa ina Wahandisi wawili (2) pekee na haina mkadiriaji majenzi hata mmoja (1) ambao ni wataalam muhimu kwa ajili ya kutathmini gharama za miradi hiyo kwa ufanisi; Ukaguzi ulibaini pia kuwa kuchelewa kukamilika kwa miradi kwa wakati ilikuwa kinyume na masharti ya mikopo. Mira...